Unordered List

Definition List

Venessa Mdee Akiri Kuwa Nyimbo Yake Mpya Ya 'Hawajui' Ilikuwa Dedication Kwa Mahasimu Wake


Vanessa Mdee amesema aliachia wimbo wake ‘Hawajui’ ulioandikwa na Barnaba baada ya baadhi ya watu kudai hakustahili kushinda tuzo ya wimbo bora wa rnb (Closer) kwenye tuzo za Kili mwaka huu.

Vee Money amesema hayo kwenye mahojiano na gazeti la Daily Nation la Kenya. “Hawajui unawahusu ‘wasema hovyo’. Hivi karibuni nilishinda tuzo za Kilimanjaro kwa wimbo bora wa R-n-B wa mwaka ambao ni wazi mashabiki wangu waliniwezesha na walifurahi sana. Lakini watu wengine wengi walisema “Oh hayukotayari, hastahili’. Hilo lilinihuzunisha. Ulikuwa ukosoaji mkubwa wa kwanza kwangu kama mwanamuziki.

Hivyo hiyo ilinisukuma kuandika kitu kuhusu watu wenye chuki lakini sio katika hali ya kawaida kwamba na wewe pia unawachukia wale wanaokuchukia,” alisema.By Bongo5
Venessa Mdee Akiri Kuwa Nyimbo Yake Mpya Ya 'Hawajui' Ilikuwa Dedication Kwa Mahasimu Wake Venessa Mdee Akiri Kuwa Nyimbo Yake Mpya Ya 'Hawajui' Ilikuwa Dedication Kwa Mahasimu Wake Reviewed by Admin on Monday, July 07, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.