Unordered List

Jokate Atafuta Mchumba, Vigezo Vyake Tatizo

Definition List

Katika kuonyesha amechoshwa na upweke, mwanamitindo Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ ameibuka na kusema kuwa sasa anasaka mwanaume wa kumuoa huku akitaja vigezo vyaanayestahili kumuita mume.

Akizungumzia maisha yake ya kimapenzi, Jokate alisema kuwa hana ‘mtu’ ila atakapotokea mwenye vigezo anavyotaka, hatakuwa na sababu ya kumkataa.

“Kwa sasa sina mpenzi wala mchumba, akitokea sina kipingamizi ila mbali na vigezo vingine awe na mapenzi ya dhati na mimi,” alisema Jokate.

Jokate amekuwa msiri sana katika maisha yake ya kimapenzi kiasi cha wengi kuamini ni msichana anayejiheshimu sana ila aliwahikuwa na uhusiano na mchezaji wa mpira wa kikapu, Hasheem Thabeet anayekipiga kwenye Timu ya Oklahoma City Thunderya nchini Marekani.
Jokate Atafuta Mchumba, Vigezo Vyake Tatizo Jokate Atafuta Mchumba, Vigezo Vyake Tatizo Reviewed by Admin on Friday, July 25, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.