STAA wa filamu Bongo, Rose Ndauka amefunguka kuwa kwa sasa yeye na msanii mwenzake, Jacqueline Pentzel ‘Jack Chuz’ ambaye aliwahi kukwaruzana naye wameshamaliza na kujikita katika kazi zaidi.
Akichonga na paparazi, Rose alisema wamerudi kwa staili ya tofauti kwani kila mmoja anafanya kazi zake lakini wanashirikishana na wana ‘project’ maalum ambayo wataifanya hivi karibuni.
“Mimi na Jack kwa sasa tunafanya kazi hata Wema ambaye tulikuwa naye kwenye kundi moja tukiwa na filamu ya kumshirikisha tutamuita kwa sababu hatuna kinyongo kwani bifu hazijengi kikubwa tunafanya kazi tu,” alisema Rose.
Rose na Jack Chuz walipishana kipindi cha nyumana chanzo kikidaiwa kuwa ni kuibiana mabwana lakini hivi karibuni walimaliza tofauti ambapo walionekana pamoja kwenye msiba wa aliyekuwa muongozaji wa filamu nchini, George Otieno ‘Tyson’.
Rose Ndauka Adai Kuacha Bifu Na Jack Chuz
Reviewed by Unknown
on
Thursday, July 10, 2014
Rating:
No comments:
Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!
Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano