Unordered List

Definition List

Prezzo Ndiye Msanii Tajiri Zaidi Afrika Mashariki Baada Ya Hili Tukio


Kwa muda sasa kumekuwa na majadiliano kuhusu nani ndiye msanii tajiri zaidi kanda ya Afrika Mashariki huku wasanii kadhaa wakijitokeza kuonyesha ubabe wao.

Kuanzia kwa Octopizzo kuonyesha kiatu chake cha $200,000 hadi kwa Prezzo kuonyesha bunduki yake ya dhahabu, anzia kwa Diamond kudai hafanyi shoo chini ya Tsh. 80milioni nje ya nchi hadi kwa Jaguar kuonyesha magari yake ya kifahari.

Okay kuanzia sasa hayo yote tumeyaweka kando kwani imekuwa officially kuwa CMB Prezzo ndiye msanii tajiri zaidi kanda nzima.

Kulingana na chanzo cha karibu kilichoongea na NairobiExposed, kimedai kuwa rais huyu wa rap nchini Kenya aliweza kuweka sahihi yake kwa deal bab kubwa ambayo itamwona staa huyu kuingiza kitita cha Ksh 800milioni takriban Tsh 16 bilioni kila mwaka. Hii ni zaidi ya kiwango cha pesa za wasanii wote kuwachanganya kwa mwaka mmoja.

Chanzo kilizidi kuongea kuwa Prezzo aliweza kuweka deal na kampuni inayosambaza mafuta ya Omukuwe Energy, kampuni ya multi billion inayomilikiwa na Philip Omukuwe ambaye ni maarufu sana kwa kuwa bilionea. Inasemekana Prezzo alimaliza deal hii mwezi Machi 27.

Kiufupi Prezzo ameivuka kwa mbali mipaka ya kawaida ya wasanii kutengeneza pesa na sahizi anajivunia kuchuna kwenye matawi ya juu.

Baada kuandamwa kwa simu kuongea issue zima kuhusu deal yake kubwa Prezzo alikuwa na haya yakuseme "Where do you people get all these from, i like putting my business out of public limelight but you know what a president got to live like one and my eye on the billion mark for now. I'll be in every African country. TMT we don't sleep "

Alipojaribiwa kuongea issue zima kuwa wale wasanii waliokuwa wakishindana naye kifedha haswa Jaguar na Diamond plus wale wengine hivi ndivyo alivyodai "the president has never been in competition with anybody you can't chase your shadow and catch it. They said i couldn't afford a jaguar (akicheka) so i said you know what? let's do a jet. Time for kids to go back and breastfeed" alikejeli Prezzo.
Prezzo Ndiye Msanii Tajiri Zaidi Afrika Mashariki Baada Ya Hili Tukio Prezzo Ndiye Msanii Tajiri Zaidi Afrika Mashariki Baada Ya Hili Tukio Reviewed by Admin on Sunday, July 27, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.