Unordered List

Definition List

Mzee Small Afariki, Mwigizaji Mkongwe Alikuwa 59


Habari za kusikitisha zilizotufikia hivi punde zinaarifu kuwa Mwigizaji maarufu na mkongwe katika fani ya vichekesho nchini Tanzania, Said Ngamba maarufu kwa jina la Mzee Small (59) amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Mzee Small amefikwa na umauti majira ya saa 4 za usiku wa Juni 7, 2014 katika Hospitaliya Taifa Muhumbili.

Akiongea kwa njia ya simu mke wa marehemu, Bi Fatuma Saidi, aliithibitishia blog ya Father Kidevu , kuwa Msanii Said Ngamba hatunae.
Bi Said amesema kuwa marehemu mumewe amefikwa na umauti baada ya hali yake kubadilika jana (Juni 7) asubuhi na kumbikiza Muhimbili ambako alishinda nae akipatiwa matibabu na majira ya saa tatu usiku alirudi nyumbani na kumwacha kijana wake akimwangalia mgonjwa na ilipotimu saa tano usiku kijano huyo alirudi na kusema baba amefariki.

“Nikweli Mzee Small amefariki”….yalikuwa ni maneno machache yaliyobenba uchungu mzito kufuatia kifo cha mumewe. Mipango ya Mazishi inafanyika nyumbani kwa marehemu Tabata Mawenzi, Dar es Salaam.
Mzee Small Afariki, Mwigizaji Mkongwe Alikuwa 59 Mzee Small Afariki, Mwigizaji Mkongwe Alikuwa 59 Reviewed by Admin on Sunday, June 08, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.