Unordered List

Diamond Kuanza Kuuza Nguo Kwa Lebo Yake

Definition List

Diamond kuanza uuzaji wa nguo
Diamond Platinumz anatarajia kuingiza sokoni bidhaa za kampuni yake ya Wasafi Classic, WCB hivi karibuni ambazo ni pamoja na viatu,T.shirt,jeans na mavazi mengine ya wanaume yenye lebo ya WCB.
Akizungumza jana na Clouds E ya Clouds TV ,Diamond alisema hivi karibuni atatumiwana sample za bidhaa hizo ili azihakiki na hatimaye ziingine madukani.
“Nikweli tulikuwana na designer tofauti tofauti kutoka wasafi ‘WCB’ lakini kwasasa zitakuwa za kiume tu ,kwa wanawake zitakuwa wachache ambao wanaweza kuvaa nguo za kiume kidogo,kwa wanawake bado nisiwe muongo,lakini zipo tayari. Kwasababu nikiwa China nilikuwa nashughulikia hivyo vitu. Lakini nikifanya chini chini kidogo kwasababu sikupenda vikichelewa halafu mwisho wa siku tuje tupigizane kelele, ‘mbona mulisema hazichelewi mbona zimechewa’, alisema Diamond.


“Lakini vilitakiwa viwe tayari toka Jumatatu iliyopita,kwasababu nahakikisha quality nzuri isionekane tunafanya tu, ikabidi ichelewe. Kutakuwa viatu,jeans,kutakuwa kuna hadi boxer, T. Shirt, kofia mengi yatakuwa na mchanganyiko mchanganyiko kidogo kwasabubu vitakuwa vya vijana zaidi yaani dizaini kama wasafi tunavyovaa.”

Habari imedondoshwa kutoka Bongo5
Diamond Kuanza Kuuza Nguo Kwa Lebo Yake Diamond Kuanza Kuuza Nguo Kwa Lebo Yake Reviewed by Admin on Friday, November 08, 2013 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.