Unordered List

Definition List

Snura, Wolper, Na Aunt Ezekiel Wazuzua Mtaa Kwa Mauno Yao

Snura
Mastaa wa filamu za Kibongo wenye jina kubwa mjini, Aunt Ezekiel, Jacgueline Wolper na Snura Mushi hivi karibuni walitisha kwa kufunga mtaa kutokana na mauno waliyokuwa wakikata mbele za wapiga ngoma wa Kundi la Baikoko, tukio lililojiri Mwananyamala, Dar nyumbani kwa msanii mwenzao Vanitha Omary.

Wasanii hao waliwashangaza watu jinsi walivyokuwa wakijituma kukata mauno huku Wolper akimtunza mpiga ngoma na kumkatikia kwa staili mbalimbali zikiwemo za chumbani.

“Yaani wewe ulikosa mambo,  Snura alitoa shoo na mapacha wake utadhani alikuwa amelipwa, yaani walinogesha ngoma ya kumuaga mdogo wake Vanitha ambaye anakwenda kufunga ndoa Dodoma,” alisema sosi aliyekuwa akimsimulia mwandishi wetu.

Unaweza pia kusoma:
Mwandishi afinya makalio ya msanii kuhakikisha si bandia

Aidha, wageni waliokuwa wamealikwa eneo hilo hawakudhani kama Wolper na Aunt wangeweza kujituma vile kama walivyokuwa wakikata mauno hayo kwa sababu ustaa wote waliuweka pembeni na kujiachia kwa raha zao.
Jack Wolper
Jack Wolper
Aunt Ezekiel
Aunt Ezekiel

-Stori: Hamida Hassan, Global Publishers
Snura, Wolper, Na Aunt Ezekiel Wazuzua Mtaa Kwa Mauno Yao Snura, Wolper, Na Aunt Ezekiel Wazuzua Mtaa Kwa Mauno Yao Reviewed by Admin on Friday, November 15, 2013 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.