Unordered List

Definition List

Msanii Matonya Aonja Utamu Wa Kutekwa Nyara

Mwanamuziki nyota wa muziki wa kizazi kipya usiku wa kuamkia Jumatatu alionja joto ya kiwe baada ya kutekwa na kusurubiwa kisha kunyang'anywa kila kitu pamoja na gari yake.

Mwanamuziki huyo akiwa kwenye viunga vya Club ya usiku ya Kibo iliyopo Tegeta Jijini Dar pamoja masisita du wakila bata ghafra kundi la watu watano lilimvamia na kumkamta msobe msobe hadi nje ya ukumbi pamoja na kumrukisha kichurachura huku wakina dada waliokuwa wamendamana nao wakilia kwa uchungu kwa kumuonea huruma.

Habari zaidi toka kwa chanzo chetu kilichoshuhudia timbwiri hilo kilisema kuwa chanzo cha tukio hilo ni kudaiwa kwa Matonya na mtoto wa mjini aliyefahamika kwa jina la Evance" Huyu Evance ni mtoto wa mjini na huwa anawakopesha pesa wanamuziki mbalimbali pamoja na wasanii wa bongo movie hivyo miezi ya hivi karibuni alimkopesha shilingi laki nne msanii huyo kwa madai kuwa hakuwa na pesa ya kula bata wikiendi ambapo baada ya kumkopesha msanii alianza kuzungusha kurudisha hali iliyomfanya Evance kuchukua hatua za kumfanyia unyambilisi huo" Kilisema chanzo chetu

Hata hivyo baada ya kumkamata msanii huyo Evance alimpelekwa Oysterbay ambapo aliiacha gari na simu kwa makubaliano atakapoleta pesa hiyo atapewa gari yake.
Msanii Matonya Aonja Utamu Wa Kutekwa Nyara Msanii Matonya Aonja Utamu Wa Kutekwa Nyara Reviewed by Admin on Tuesday, November 12, 2013 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.