Unordered List

Definition List

India Kwa Mara Ya Kwanza Wametuma Ndege Yao Kwa Sayari Ya Mars

Nchi ya india kwa mara ya kwanza yapeleka ndege katika sayari ya Mars
Siku ya leo 5 Novemba imekuwa historia kuu kwa nchi ya india baada ya kutuma ndege yao kwa mara ya kwanza katika sayari ya Mars.

Nchi hii inatarajiwa kuwa nchini ambazo zimewahi kupeleka utafiti kwa sayari hiyo nyekundu.

Nchi hii ikishirikiana na shirika la utafiti wa anga waliweza kuzindua na kurusha ndege yao ya kwanza leo saa 5.30 asubuhi masaa ya afrika mashariki katika kituo cha Satish Dhawan Space Centre.

Wakifaulu katika jambo hili, nchi ya India itakuwa miongoni mwa nchi kama Soviet Union, NASA na Europeans ambao wameshawahi kutuma ndege zao katika sayari ya Mars.

Nchi ya Japan na Uchina walijaribu kurusha ndege zao lakini hawakufaulu kwa sababu ya hitilafu za mitambo.

Unaweza pia kusoma:
Nchi ya Korea Kujenga jumba lisiloweza kuonekana

Safari ya ndege hio hadi anga ya Mars itachukua takriban miezi kumi.

India katika utafiti wao wataweza kuchunguza anga ya sayari hio pamoja na madini ambayo yanapatikana katika sayari hio.

Kiongozi anayeongoza zoezi hili K. Radhakrishnan amekiri kuwa changamoto kuu ni kuwa na teknolojia ya kisasa na anafahamu kuwa awali nchi zilizojaribu kufanya zoezi hili wengine hawakufaulu.
India Kwa Mara Ya Kwanza Wametuma Ndege Yao Kwa Sayari Ya Mars India Kwa Mara Ya Kwanza Wametuma Ndege Yao Kwa Sayari Ya Mars Reviewed by Admin on Tuesday, November 05, 2013 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.