Unordered List

Definition List

Nchi Ya Korea Kujenga Jumba Lisilo Onekana

Jumba la Infinity Tower, picha iliyotengenezwa na tarakilishi
Kampuni ya GDS Architects imepewa kandarasi ya kujenga jumba lisiloonekana nchini Korea.

'Tower Infinity' litakuwa jumba la kwanza ulimwenguni lisiloweza kuonekana. Jumba hili nimepangwa kujengwa karibu na uwanja wa ndege wa Incheon, karibu na jiji kuu la Seoul, Korea Kusini.

Jumba hili halitakuwa refu ulimwengu mzima, kwani limepangiwa urefu wa mita 450. Lakini jambo lake geni zaidi ni kuwa na uwezo wa kujificha na kutoonekana.

Kwa ujenzi ni kuwa jumba hilo litatengenezwa na kuzungukwa na projectors na kamera aina ya LED. Kamera zitatumika kupiga picha mazingara yanayozunguka jumba hilo halafu picha hizo zitaunganishwa kutengeneza picha moja kuu ambayo itatumika kuangazwa na hizo projectors.

Hii ndio itasaidia jumba hilo lisiweze kuonekana.

Katika mtandao wa kampuni ya GDS inayosimamia ujenzi wa jumba hilo wamesema kuwa inataka kuonyesha dunia nzima kuwa Korea si nchi ambayo imejitokeza ionekane na kila mtu pekee bali pia kuonyesha kuwa imejitokeza isiweze kuonekana.

Kwa kuwa jumba hilo litakuwa la kimaajabu, Korea wamesema kuwa wanatarajia jengo hilo liwe kivutio cha watalii nchini humo.
Nchi Ya Korea Kujenga Jumba Lisilo Onekana Nchi Ya Korea Kujenga Jumba Lisilo Onekana Reviewed by Admin on Friday, October 18, 2013 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.