Kwa mujibu wa taarifa tulizozipata hivi punde katika habari mpasuko ya
Radio One kupitia ujumbe mfupi wa simu za mkononi kwamba, Mwandishi wa
habari na Mtangazaji wa ITV na Radio One Stereo Ufoo Saro amejeruhiwa
kwa kupigwa risasi baada ya kuvamiwa na mtu asiyefahamika nyumbani kwake
Kibamba Kinondoni Jijini Dar es salaam.
Aidha mvamizi huyo alimuua mama yake Ufoo papo hapo na yeye mwenyewe kujiua kwa risasi,
Aidha anayedhaniwa kufanya mauaji hoyo ya kutisha ni mume au mchumba wa mwandishi wa habari wa ITV na Radio One Ufoo Saro na yeye mwenyewe kujiua.
akizungumza
na mtandao huu kamanda wa polisi wa mkoa wa kipolisi wa kinondoni
kamanda Wambura amesema tukio hilo limetokea majira ya alfajiri ya leo.
Kamanda
wambura ameongeza kuwa mwanaume huyo anafanya kazi umoja wa mataifa UN
huko sudani ila bado haijafahamika kwamba anafanyia kitengo gani (japo kwa habari za mtaani zinasema mtu huyo ni mwanajeshi ila bado hazijathibitishwa)
Kamanda
Wambura anasema inasemekana kulikua kuna ugomvi kati ya wawili hao
ambapo walishindwa kuelewana na ndipo walipoamua kwenda kwa mama mzazi
wa Ufoo Saro(mama mkwe) na ndipo mwanaume huyo alipomshutumu mama mkwe
wake kwamba anamtetea mwanae ndipo alipotoa bastola na kumpiga mama yake
na Ufoo Saro Risasi ya kichwa na kumuua papo hapo na kisha akampiga
Ufoo Saro risasi ya mbili moja ya tumboni na ingine ya mguuni na kudhani
kwamba amemuua kumbe amemjeruhi tu kisha kujipiga mwenyewe risasi ya
kidevuni na kufariki dunia hapo hapo.
Habari hii imedondoshwa kutoka Tuangaze Bongo
Mwandishi Wa Habari Wa ITV & Radio One Ufoo Saro Apigwa Risasi. Mamake Auawa
Reviewed by Admin
on
Sunday, October 13, 2013
Rating:
No comments:
Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!
Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano