Unordered List

Definition List

Mechi Ya Simba Na Yanga Yafaidi Zaidi Ya Sh 500,000,000



Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) ya watani wa jadi Simba na Yanga iliyochezwa Jumapili (Oktoba 20 ) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es salaam na kumalizika kwa sare ya mabao 3-3 imeingiza sh. 500,727,000. 
Mashabiki 57,422 ndio waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo nambara 63 kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na sh. 30,000. 
Kulibakia tiketi 131 tu ambazo hazikuwe kuuuzwa zikiwa 90 za VIP A, 40 za VIP B na moja ya VIP C. Tiketi zilizochapwa kwa ajili ya mechi hiyo ni 57,558 ambayo ndiyo idadi ya viti vilivyopo kwenye uwanja huo. 
 Kila klabu imepata mgawo wa sh. 123,025,564.32 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 76,382,084.75. 
Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 62,555,371.69, tiketi sh. 7,309,104, gharama za mechi sh. 37,533,223.01, Kamati ya Ligi sh. 37,533,223.01, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 18,766,611.51 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 14,596,253.39.

Unaweza pia Kusoma:
Fastjet Yaingia Katika Kumbukumbu

Boniface Wambura Mgoyo, Ofisa Habari Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) alitoa takwimu hii.

Mechi Ya Simba Na Yanga Yafaidi Zaidi Ya Sh 500,000,000 Mechi Ya Simba Na Yanga Yafaidi Zaidi Ya Sh 500,000,000 Reviewed by Admin on Tuesday, October 22, 2013 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.