Unordered List

Definition List

Fastjet Kwa Mara Ya Kwanza Yaingia Katika Historia

Siku ya Ijumaa kampuni ya Fastjet iliingia katika kumbukumbu ya kwanza kufanya safari ya kwanza nje ya Tanzania.

Ndege aina ya FN201 ilitua katika uwanja wa ndege wa Johannesburg Tambo International airport kutoka uwanja wa Julius Nyerere saa 5.25 asubuhi.

Kampuni ya ndege za Fastjet ni moja wapo ya kampuni ambayo hutoa huduma ya usafiri kwa bei nafuu sana. Wamiliki wa ndege hizi ni Fastjet Plic ambayo ni ya Uingereza.

Lengo kuu la kampuni hii ni kutoa huduma kwa bei nafuu africa nzima.

Kampuni hii ilijeuza jina baada ya fly540 kushindwa kushindana na kampuni nyigine kuu za ndege. Kampuni hizo za ndege nchini Ghana, Kenya na Angola hazijaleta faida zozote na mwaka wa 2012 waliamua kubadilisha jina hadi Fastjet.

Safari za kutoka Dar es salaam zitakuwa mara tatu kwa wiki, Jumatatu, Jumatano na Ijumaa. Bei ya safari hizo ni nusu ya safari ya ndege nyingine kwa $345 safari moja.

Wasafiri waliotumia ndege ya Fastjet katika safari ya Fastjet walisema kuwa safari hio ilikuwa nzuri bila shida yeyote huku wakipongeza Fastjet kwa kurahisha usafiri wakijali maslahi ya wananchi wa kawaida.

Wakuu wa kampuni ya Fastjet wameshindwa kujieleza kuwa ndege hizo ni nafuu zaidi ukilinganisha na ndege aina yeyote.
Fastjet Kwa Mara Ya Kwanza Yaingia Katika Historia Fastjet Kwa Mara Ya Kwanza Yaingia Katika Historia Reviewed by Admin on Sunday, October 20, 2013 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.