Unordered List

Definition List

Jeshi La KDF Lilihusika Na Wizi Katika Jumba La Westgate

Duka la airtel baada ya kuporwa bidhaa zote. Simu zote katika duka hilo ziliibiwa
Nairobi. Sasa imebainika kuwa uokoaji katika duka la Westgate ulikuwa na kasoro. Hii ilibainika baada ya wamiliki wa maduka walipoachwa vinywa wazi baada ya kupata mali zao zimeporwa.

Inaaminika hizo siku nne wanajeshi waliokuwa wakikabiliana na magaidi walikuwa wakipora mali za wenyewe. Video ambazo zimewanasa wanacheshi hao zimetolewa.

Baada ya operesheni hiyo kukamilika, wafanyakazi katika duka la Airtel walishikwa na butwaa baada ya kupata duka lao liko wazi na hakuna chochole kilichobakishwa. Simu zote, laptops, tablets na bidhaa zote katika duka hilo zimeporwa. Hata zile simu butu za kuonyesha zimeibwa. Kile kilichoonekana ni nguo ambazo zimetoka katika maduka mengine. Inakisiwa wanajeshi hao waliziacha nguo hizo hapo baada ya kuligundua hilo duka na kutaka kubeba vitu vyepesi.

Maduka mengine pia hayakusazwa, maduka yote katika orofa ya kwanza hadi ya tatu yalikuwa yamefugwa lakini wengi waliyapata yakiwa wazi. Mmoja wa wanabiashara ambaye anauza saa za Rolex na dhahabu pia alilipata duka lake liko wazi na hakuna kitu ndani. "Tulifunga maduka yetu tukiamini KDF wanakabiliana na magaidi hao lakini kumbe ilikuwa ndivyo sivyo." aliongea mmoja.

Kulikuwa na uhakika kuwa KDF walihusika kwa sababu kulionyesha risasi ambazo zilitumika kuvunja vioo vya bulletproof katika duka hilo la kuuza saa za Rolex. Kuna wengine wanadai kuwa vilipuzi vilitumika ili kuwezesha wezi hao kuiba bidhaa hizo.

Inasemekana kwa siku mbili KDF hawakuwa wakikabiliana na magaidi wowote kwani walitoroka kupitia katika mtaro mmoja ambao unaunganisha Westgate na jumba jingine la Nakumatt Ukay. Magaidi hao walitoroka masaa machache baada ya majeshi hao kulizunguka jumba hilo.

Cha kushangaza katika tukio hilo la Westgate, wanahabari walisukumwa mbali kutoka jumba hilo na hakukuruhusiwa kupigwa picha. Magari ya kubeba wagonjwa yanaaminika ndio yaliyotumika kusafirisha mali hizo walizopora.

Wanajeshi hao walipata nafasi ya kutoka duka moja hadi jingine, banki moja hadi nyingine wakipora mali iliyokuwa nyingi kupindukia. Tayari banki ya Barclays pamoja na Millionaires Casino wameandikisha taarifa kwa polisi kuwa wamepoteza KShs 2.9 milioni kwa wezi wa KDF.

unaweza pia kusoma:
Kesi Ya Papaa Msofe Yapamba Moto Kortini
Al Shaabab Yaingia Tanzania?

Kujaribu kuziba ushahidi wa wizi wao, walichoma magodoro katika duka la Nakumatt humo ndani wakiwahadaa wananchi kuwa ni magaidi hao. Pia walipiga bomu sehemu flani katika jumba hilo na kuporomosha orofa nzima. Inaaminika zaidi ya watu 70 walipoteza maisha yao kiholela baada ya KDF kuchukua jukumu la kukabiliana wa magaidi hao.

Wakuu wa polisi wanaamini itakuwa ni gaidi mmoja pekee ndie aliyopoteza maisha yake kwani wale wengine walitoroka. Mpaka sasa hakujatoka ripoti yeyote inayoashiria kuwa kuna maiti zozote za magaidi hao.

Kitengo cha polisi cha Recce Squad kilisikitishwa na tabia ya KDF kwani wao ndio walipewa jukumu la kufanya uokoaji huo lakini pindi jeshi lilivyokuja, walikuwa na ajenda fiche na kulazimisha kuchukua uongozi na kudhalilisha kitengo hicho cha polisi.

Maafisa wa Israel Defense Force(IDF) walikataa kusaidiana na KDF kwani walijua kitengo cha Recce Squad ni kamili na kimepokea mafundisho nchi ya Israel.

Jambo hili limemghadhabisha rais wa nchi hio Uhuru Kenyatta na kulaumu idara ya usalama kuwa imejitenga na serikali na kufanya mambo kichinichini. Rais ameamua kufanya mabadiliko ya dharura katika idara yote ya usalama.
Jeshi La KDF Lilihusika Na Wizi Katika Jumba La Westgate Jeshi La KDF Lilihusika Na Wizi Katika Jumba La Westgate Reviewed by Admin on Saturday, October 12, 2013 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.