Unordered List

Definition List

Al-Shabaab Yaingia Tanzania!?

Mtwara. Siku ya jumatatu iliwashtua wakaazi wa Mtwara baada ya kugunduliwa genge la watu lililojificha katika msitu wa mlima wa Mkoliongo wakifanya mazoezi ya kivita. Wanaume wachangamfu kumi na mmoja waliokuwa kati ya miaka 18-39 walikamatwa wakipata mafunzo ya kigaidi. Vijana hao walikamatwa wakiwa na CD 25 za video pamoja na vifaa aina kadhaa za kimafunzo.

Al-Shaabab ni kundi ambalo limejihusisha na mashambulizi kadhaa nchini Kenya na shambulizi la mwisho lilifanyika Westgate ambapo watu zaidi ya 65 walipoteza maisha yao.

Kulingana na Kamanda wa polisi mkoa huo Zelothe Stephen, alisema kuwa vijana hao walipatikana na CD zikiwemo kuonyesha matukio ya kigaidi yaliyofanywa na al-shabaab, mauaji ya Osama bin Laden na rais wa zamani wa Uganda Iddi Amin. Pia katika CD hizo kulikuwemo na 'Zinduka Zanzibar'.

Inaonekana vijana hao walikuwa kwa msitu huo kwa kujipanga kwani vifaa kama mashine za DVD, solar power panels, betri, visu, jiko la makaa,baiskeli kadhaa na bidhaa nyingine zilipatikana.

unaweza pia kusoma:
Director wa Kibongo Anaswa akila Uroda

Uzuri ni kuwa polisi wamekabiliana na vijana hao na wamechukuliwa kupelekwa mahakamani kusaidia polisi na uchunguzi zaidi.

Al-shabaab chimbuko lake ni Al-Qaeda lakini walijitenga baada ya mgogoro wa uongozi baina ya makundi hayo mawili.
Al-Shabaab Yaingia Tanzania!? Al-Shabaab Yaingia Tanzania!? Reviewed by Admin on Tuesday, October 08, 2013 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.