Unordered List

Definition List

Vyakula Aina Kumi Vya Kujenga Misuli

Kujenga misuli ni kitu ambacho wengi wangependa kufanya katika maisha yao. Kuwa na misuli mwilini husaidia pakubwa kufanya mtu kuseza kuinua mizigo mizito bila shida yeyote. Kuwa na misuli pia hufanya mtu kuweza kuwa na mwili ambao hujikinga wenyewe kutokana na magonjwa ya mara kwa mara na pia humuezesha mtu kuwa na mwili wa kuvutia.

Lakini tatizo kuu ni kuwa wengi hawajui mbinu bora ya kujenga misuli na hujitweka na majukumu ya kuinua vyuma vizito na kufanya mazoezi mazito kwa miili yao ili kuwa na misuli. Hivi vitendo kimsingi husaidia lakini pia huumiza mwili kama hutatumia vyakula vinavyohitajika kujenga misuli.

Ni muhimu kwa mtu kuelewa vyakula gani vinavyohitajika katika kujenga misuli na pia kujiepusha na vyakula ambavyo vitakuletea mafuta yasiyokuwa na manufaa kwa mwili.

#1. Nyama isiyokuwa na mafuta
Nyama ya kuku isiyokuwa na ngozi wala mifupa husaidia sana kwa kuupatia mwili wako nguvu ili kuendesha shughuli zote zinazohitajika katika mwili wako.

#2. Samaki
Samaki ni muhimu sana haswa tilapia.Wana asilimia kubwa ya protini na fatty acid ambayo mwili huhitaji kwa wingi lakini haiwezi hutengeneza. Inasaidia sana kulisha misuli yako na kupunguza kiwango cha mafuta mwilini.


#3. Soy Protein
Haya madini hupatikana kwa kutenganisha mbegu za soya na hupatia mwili wako kiwango kikuu cha protini.

#4. Protein Shake
Huu ni mchanganyiko wa protini, mafuta na cabohydrates ambazo hukupatia nguvu ambazo hukufanya usishikwe na njaa kwa muda mrefu. Husaidia pakubwa kwa kujenga misuli. 

#5. Maharagwe
Maharagwe ni muhimu na njia rahisi ya kupatia mwili protini. Maharagwe kama ya soya, maharagwe meusi na yale ya 'kidney beans' yana kiwango kidogo cha  mafuta na hupatia mwili wako aina tofauti za carbohydrate, husaidia kuhimidi kiwango cha sukari na kupunguza uhitaji wa sukari kwa mwili wako.

#6. Cottage Cheese
Hii husaidia kuongeza misuli kwa mwili wako. Ni muhimu kwa mwili.

#7. Mboga
Mboga kama mrenda, mchicha, mboga za mkunde na nyinginezo huupa mwili kiwango kikubwa cha maji, madini na pia 'fibre' ambayo hujaza caloria ambazo zimepotea kwa mwili wako.

#8. Matunda
Matunda yana kiwango kikubwa cha nutrients pamoja na fibre.

#9. Oatmeal
Hii husaidia mwili wako na fibre pamoja na kusaidia kuendesha shughli za mwili wako. Hupunguza haraka ya kusaga chakula ambavyo husaidia kuufanya mwili kuhisi kuwa umeshiba kwa muda mrefu. Pia huchangia kupunguza mafuta.

#10. Maji
Maji ni muhimu zaidi kwa mwili kwa sababu mwili ukikosekana kwa mwili utafanya misuli yako iwe membamba kwa sababu ya kutoa maji ili kusaidia kuupatia mwili maji. Maji ni kitengo muhimu katiika mwili.

Vyakula Aina Kumi Vya Kujenga Misuli Vyakula Aina Kumi Vya Kujenga Misuli Reviewed by Admin on Saturday, October 05, 2013 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.