Unordered List

Definition List

Diamond Mwanamziki Anayelipwa Zaidi Afrika Mashariki

Diamond Platinumz ndani ya limousine wakati alipokuwa jiji la Mombasa.
Mwanamziki huyu amejitosa kwa ulingo wa mziki na sahizi amefauli kimziki. Diamond kwa jina la kuzaliwa anaitwa Nasib Abdul mwenye umri wa miaka 24. Amefanikiwa kimziki na kuweza kuwashinda wakongwe wa mziki ambao wamekuwa hapo katika music industry zaidi ya miaka kumi.

Diamond ameweza kuteka hizia za afrika mashariki kwa nyimbo zake za bongo flava. "Si rahisi kwa mwanamziki kujeuza jinsi watu wanavyosikiliza miziki flani." Jamaa mmoja shabiki wa mwanamziki huyu alisema wakati Diamond alipozuru Nairobi. Kulingana na wadaku, inasemakana Diamond alipokuwa Kenya kufanya show zake, kila show moja alikuwa akitoka na zaidi ya KShs 1.5million. Hili ni jambo ambalo si rahisi kwa msanii wa kawaida kulifanya.

Kabla Diamond kuibuka, msanii Chamellion ndie aliyesifika kuwa na pesa nyingi lakini kwa sasa mambo yamebadilika.

Kuonyesha umaarufu wa Diamond, kila anapotoa nyimbo yeyote lazima iingie kwa chart na kuchezwa kwa vyombo vya miziki kanda hii ya afrika mashariki. Video yake mpya ya Number Moja iliyotengenezwa na Ogopa Videos ilizua hisia tofauti tofauti na wengi waliisifu kuwa ni video ambayo haijawahi kutengenezwa mfano wake kanda hii na jambo hili limechangia kuangaliwa zaidi ya mara nusu milioni katika youtube tangu izinduliwe. Haijajulikana kiuhakika video hio ilimgharimu mwanamziki huyu pesa ngapi lakini si pesa kidogo unavyofikiria.

Ingawa mwanamziki huyu anafanya vyema kimziki, kuna mahasidi wake ambao wako mstari wa mbele kumuharibia jina kuwa yeye ni mmoja wa wale wanaosemekana ni illuminati. Diamond amekana tetesi hizi na kusisitiza kuwa hizo zote ni porojo.
Diamond Mwanamziki Anayelipwa Zaidi Afrika Mashariki Diamond Mwanamziki  Anayelipwa Zaidi Afrika Mashariki Reviewed by Admin on Tuesday, October 08, 2013 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.