Unordered List

Definition List

Barobaro Amlilia Mamake Baada Ya Viboko Kuzidi Unga

Barobaro ambaye ni shabiki sugu wa Manchester City alikiona cha mtema kuni baada ya kuchapwa viboko hamsini hadharani. Jamaa huyu aliagana na mashabiki wa Bayern Munich kwamba kama wangeweza kuwafunga the Blues basi mwili wake ungekuwa halali yao. Kama kawaida watu humiminika katika mkahawa fulani unaopatikana sehemu fulani mjini Tabora. Mechi kabla haijaanza barobaro huyu alikuwa akiwafokea mashabiki wa Bayern kwa matusi huku akiwadhalilisha mbele ya watazamaji wengine wa mpira huo. Mashabiki hao waliudhiwa mno na maneno yaliyotoka kwa kinywa cha barobaro huyu.
Mpira ulipoanza tu na Mchezaji Ribery alipofunga bao la kwanza ilimnyamazisha jamaa huyu. Alipoona ManCity wamelemewa alitaka kujiondoa kwa kukimbia lakini aliambulia patupu kwani alizungukwa na mashabiki hao huku wakighadhabishwa na maneno aliyoyasema awali.
Punde tu kipenga kilipopulizwa kuashiria kuwa mpira umeisha jamaa huyu alianza kupiga mayowe huku akitaja jina la mamake lakini haikumsaidia kwani maji yashamwagika. Bila huruma mashabiki hao walimvamia na viboko huku wengi wakimzomea na kumcheka. Ilikuwa kizaaza kikubwa ambacho kilifanya majirani waliokuwa wanaishi karibu na mkahawa huo kuamka na kutaka kujua kitu gani kilichokua kikiendea.
Barobaro Amlilia Mamake Baada Ya Viboko Kuzidi Unga Barobaro Amlilia Mamake Baada Ya Viboko Kuzidi Unga Reviewed by Admin on Thursday, October 03, 2013 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.