Dar es Salaam. Balozi anayeondoka wa marekani Alfonso Leihardt alimtembelea rais Jakaya Kikwete ikulu kwenda kumuaga kirasmi baada ya kumaliza miaka miine ya kidiplomasia nchini. Leihardt alimtakia Kikwete sherehe njema anaposherehekea siku yake ya kuzaliwa.
Rais aliupongeza ushirikiano baina ya Tanzania na Marekani akisema kuwa uhusiano baina ya nchi hizo mbili umefanikishwa zaidi na balozi huyo.
Rais aliongezea kuwa kuwepo kwa Leihardt miaka minne Dar es Salaam kumeleta mafanikio kiuchumi na kidiplomasia katika sekta kadhaa.
"Nakushukuru kwa kazi nzuri uliyoifanya katika miaka yako minne hapa katika hii nchi. Mambo kadhaa katika uongozi wako yamefanikiwa ili kufaidi nchi hizi mbili." rais Kikwete alimwambia Leihardt.
Anaamini kuwa uongozi mpya wa balozi ya marekani utakaokuja utaendeleza pale bw.Leihardt alipoacha. Leihardt alisema kuwa moyo wake popote pale atakapoajiriwa utabakia Tanzania na anaishukuru nchi ya Tanzania kwa ushirikiano uliyotoa.
Baada ya kupiga gumzo, Leihardt alichukua nafasi ya kumtakia Kikwete maisha marefu. Katika kikao hicho pia kilihudhuriwa na Mama Salma na Mama Jacqueline Lenhardt.

JK: Umetuletea Mafanikio Kiuchumi Na Kidiplomasia
Reviewed by Admin
on
Tuesday, October 08, 2013
Rating:
No comments:
Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!
Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano