Dodoma. Mahakama imemfungulia mashtaka Mtemi Dinda baada ya kumuoza bintiye wa umri wa miaka 11. Kulingana na Mkuu wa Wilaya ya Baha, Betty Mkwasa, mzazi huyo alishtumiwa kwa kumuoza bintiye mwezi wa September kwa mahari ya mbuzi 13. Jamaa ambaye alitakiwa kumuoa binti wa mzee huyu anajulikana kama Omari Nkwani.
Mkwasa aliendelea kusema ya kuwa mhutumiwa huyo amefikishwa mahakamani kwa kosa la kumuoza mwanawe wa miaka kumi na moja. "Serikali imekuwa ikipigana vita ndoa za utotoni kwani zimekuwa na athari kwa watoto wa kike." alisema huku akionyeshwa kutopendeza na kisa hicho. Mkuu huyo ameanzisha mikakati ya kuwatafuta mama mzazi na yule bwana aliyetakiwa kumuoa binti ambao wako mafichoni.
Tabia ya kuwaoza watoto wadogo imekithiri sana wilaya hio na Mkwasa ameonya kuwa kukamatwa kwa Mtemi Ndinda kutakuwa ni funzo wa wazazi wengine. Mkuu huyu alilalamika kuwa wazazi wameingiwa na tamaa ya kujinufaisha wenyewe bila kuyafikiria maisha ya watoto wao wa kike.

Afikishwa Kortini Kwa Kosa La Kumuoza Bintiye Kwa Mahari Ya Mbuzi 13
Reviewed by Admin
on
Wednesday, October 09, 2013
Rating:
No comments:
Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!
Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano