Baada ya wiki moja kufungwa baadhi ya vyombo ya habari vikiwemo Mwananchi na Mtanzania, Stolla ameamua kusitisha kimya chake kwa kusema kuwa serikali kufungia vyombo ya habari ni jambo lililopitwa na wakati na kusema sheria ya usalama ya mwaka wa 1970 imepitwa na wakati. "Katiba tu hutoa miongozo ya jumla ya uhuru wa habari,...Tuna uhuru wa vyombo vya habari, lakini tatizo lipo hasa katika sheria zinazosaidia utekelezaji." aliendelea kusema.
Serikali iliamua kufungia magazeti haya mawili kwa sababu ilisemekana kueneza uvumi na kuchochea watanzania. Mwananchi limefugwa kwa muda wa siku 14 ilhali Mtanzania limefungwa kwa siku 90.
Jambo hili lilizua hisia na wadau mbalimbali wamelalamikia hatua hiyo kwa kuikosoa serikali kuwa inaifungia uhuru wa wanahabari pamoja na kuficha mambo yanayotendeka ndani ya serikali. Asasi 50 za kiraia ziliungana mikono kulaani hatua hio na kusema kuwa serikali imechukua hatua hii ili kuendeleza uovu na kuzima uhuru wa mwananchi wa kawaida.
Jambo hili pia liliwaghadhabisha muungano wa ulaya na msemaji wa umoja huo, Tom Vens akiungwa mkono na balozi wa Canada, Norway na Uswizi waliolaani hatua hio.
Hii mitindo ya kukandamiza vyombo ya habari afrika vimeenea ikiwemo maandano yaliyofanyika nchini Afrika Kusini kupinga serikali kwa kunyamazisha wanahabari. Pia nchini Kenya jambo la kugandamiza vyombo vya habari vimekuwepo.

Fransis Stolla: Sheria Ya Magazeti Ya Mwaka 1976 Umepitwa na wakati
Reviewed by Admin
on
Sunday, October 06, 2013
Rating:
No comments:
Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!
Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano