Unordered List

Definition List

Nabii Anayetibu Ugonjwa Wa UKIMWI amulikwa!

Nairobi. Visa vya wahubiri kuhadaa waumini wao vimeongezeka sana jijini Nairobi. Kila mtu hutafuta njia ya jinsi atakavyoweka mkate mezani nyumbani kwake wakati jua litakapozama. Uchumi umezoroteka na kila mtu atafanya hila yeyote ili kuona amefanikawa kimaisha, na njia rahisi imeonekana kuwa ni kufungua kanisa.

Kutana na Dkr. Nabii Victor Kanyari ambaye anaweza kutibu ugonjwa wa ukimwi, kufanya upate kazi, ufanikiwe kimaisha, kukuwezesha upate mtoto na hata ubarikiwe na mpenzi mwema kwa kutumia jina la Yesu na kitabu cha Biblia. Nabii huyu ni maarufu sana kwa kipindi chake kinachoangaziwa katika runinga ya KISSTV nchini Kenya.

Alijipatia cheo cha nabii huku akisema kuwa ametumwa na mungu mwenyewe kuja kutibu magonjwa na kutatua matatizo hapa duniani ila tu ushirikiane naye. Ingawa anadai ametumwa na mungu kuponya, yeye hafanyi kazi yake bure, lazima utoe ada fulani ya huduma zake.

Nabii huyu katika kanisa la Salvation Healing Ministry kila mahubiri yake analenga vifungu katika biblia ambavyo vinasema watu kutoa, na amejikita na misimamo hii kuwa lazima utoe ndio ubarikiwe. Katia runinga anasistiza kila baada ya dakika tano kuwa lazima utoe pesa kwa namba za mpesa alizoziweka kwenye runinga. Toa sadaka fulani ili utibiwe ugonjwa fulani.

Pia ameweza kupata wafuasi ambao wamefundishwa na kuandaliwa ili kutoa ushuhuda wa uongo eti walitoa maelfu ya mapesa kanisani ndipo wakafanikiwa kimaisha.

Kitambo kidogo mwanahabari wa uchunguzi maarufu ajulikanae kama Mohamed Ali, alipata kufichua siri za wahubiri hawa kuwa wanatumia madanguro na malaya wa mijini ili waje kutoa ushuhuda wa uwongo makanisani.

"Serikali haijachukua hatua yeyote ya kuhakikisha makanisa mapateli yote yamefungwa. Wanahadaa waumini wasiojielewa kwa kuwateka hisia zao na kufyonza mali zao kiholela." mmoja ambaye alikuwa mwathiriwa wa kanisa la nabii Kanyari aliongea baada ya kugundua ujanja. "Sisi huenda makanisa hayo kana kwamba tumepofuka macho, tuna macho lakini hatuoni, tuna masikio lakini hatusikii." aliongezea.

Nabii huyu mwezi Agosti alizua hisia kali katika mitandao ya kijamii nchini Kenya baada ya kumtembeza uchi mtoto ambaye alikuwa ameathirika na ugonjwa wa UKIMWI huku akiomba watazamaji watoe pesa ili mtoto huyo aweze kuombewa.

"Ukweli ni kuwa biashara ya kufungua kanisa mjini Nairobi ni nzuri na muda mfupi utaweza kununua jumba bora tu uwe na kipawa cha kuteka hisia za waumini." alisema mmoja wa waumini katika kanisa hilo la Salvation.

Kuna mtangazaji mmoja wa NTV Kenya alitaka kujua ukweli wa huyu nabii na aliamua kumpigia simu na kumwambia kuwa anahitaji maombi ya kupata mtoto. Nabii huyu bila aibu alimtaka aje kwa nyumba yake usiku ili ambariki. Katika mazungumzo ya simu nabii huyu alisikika akisema hivi "Wewe si unataka mtoto? Njoo leo nyumbani kwangu ili upate mtoto wa kipasta, si unatamani mtoto wako awe mhubiri?"

Baada ya habari ya kanisa hilo kufichuliwa kuwa ni tapeli, haikuzuia waumini hao kutoenda kwa kanisa hilo bali ilichangia kuwa maafuru na sahizi nabii huyu ameongeza ada ya maombi yake, labda hii ni kwa sababu ya ongezeko la ushuru katika bidhaa fulani nchini humo.

"Siku hizi huku hakuna kuamini mwenzako, huwezi kujua unaabudu mungu au shetani. Jiamini wewe mwenyewe na usiamini mwenzako kwani unaeza potoka." Maneno haya yalizungumzwa na askari mmoja wa usalama wiki iliyopita Bandarini Mombasa baada ya kupatikana shehena iliyojaa fuvu, mifupa na miili ya binadamu iliyokusudiwa kuingia nchini humo.

Mambo na ushirikina umejaa nchi humo kufikia kiwango cha kuwa makanisa kadhaa na wanamuziki wa injili wanashukiwa kutumia vibaya vipawa vyao kwa shetani ili kunasa wananchi wasiolewa chochote.
Nabii Anayetibu Ugonjwa Wa UKIMWI amulikwa! Nabii Anayetibu Ugonjwa Wa UKIMWI amulikwa! Reviewed by Admin on Monday, October 14, 2013 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.