Unordered List

Definition List

Mamake Diamond Platinumz Amkana Wema

MAMA mzazi wa msanii wa nyimbo Number One, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Sanura Kasim ‘Sandra’ ameingilia kati penzi lililofufuka upya kati ya mwanawe na staa wa filamu za Kibongo, Wema Sepetu. Habari za CHUMBANI zimesemaa kuwa baada ya kuambiwa na kuoneshwa picha za Diamond akiwa kimahaba na Wema alikuja juu akidai kuwa hamtaki Wema Sepetu kutokana  na tabia  zake na  kudai kuwa Penny  ndo chaguo halali la Diamond.

Akizungumza na GPL nyumbani kwake Sinza- Mori jijini Dar wikiendi iliyopita, mama huyo alisema kuwa kwa sasa hafahamu chochote kuhusu Diamond kurudiana na Wema zaidi ya kusikia kwa watu na kuona picha katika mitandao ya kijamii. “Kuhusu Nasibu  kurudiana na Wema, nasikia tu na kuonyeshwa picha namsubiri Nasibu arudi kisha nikae naye ndipo nitatoa msimamo wangu,” alisema mama huyo.

Mwandishi huyo kadiri alivyozidi kumchimba mama mkwe huyo wa Wema ni jinsi gani anavyojisikia kuhusu tabia ya kubadilisha wanawake kama nguo, ikizingatiwa yeye ni mzazi haoni kama mwanaye anamfedhehesha alisema kuwa hayo ni maisha yake. “Hayo ni maisha yake mwenyewe kwa kuwa ameshazoea kuonekana katika magazeti kila wakati mi niongee nini wakati ndiyo maisha aliyojiwekea,” alimalizia kusema.

Imedondoshwa kutoka issadody blog
Mamake Diamond Platinumz Amkana Wema Mamake Diamond Platinumz Amkana Wema Reviewed by Admin on Wednesday, October 16, 2013 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.