Unordered List

Definition List

Kutana Na Wanaume Ambao Wako Tayari Kupokea Ukimwi

Kundi hili la wanaume linalojiita 'bug chaser' lilianzishwa Marekani na kimeanza kupata wafuasi wake ulimwenguni mzima. Watu hawa wako tayari kupoa na kusambaza ugonjwa huu wa UKIMWI kwa kila ambaye ataridhika. Kundi hili lengo lake kuu ni mtu kupata raha kwa njia ya kuogofya.

Sahizi mamia ya wanaume katika mitandao ya kijamii ikiwemo mtandoo wa 'bug chaser personal' wamejitokeza kutafuta na kusambaza ugonjwa huu kwa yeyote yule. Kwa hawa 'bug chasers' ugojwa huu wanauchukulia kama zawadi - jambo ambalo mwanamume yeyote anafaa kupokea na kusambaza kupitia ukuzaji wake kisiri.

Wengine wanajishasha kuwa ugonjwa huu unawapatia muda mzuri wa kujitunza kwani matumizi ya lishe bora na kujiangalia vyema kiafya ndio chanzo cha kujipatia ugonjwa huu.

Mwanamume mmoja katika hilo kundi ajulikanae kama Nick anasema, "Mimi najihisi mchangamfu na mwenye nguvu baada ya kuanza matibabu. Sina jambo lolote la kunisikitisha kama nimepata ama kupatwa na ugonjwa huu. Jambo moja tu kupata ugonjwa huu ni kuwa kuna raha nyingine hupotea.

Nick anadai ameshawahi kufanya ngono bila kinga na wanaume zaidi ya 1,000 wakati alipokuwa akiutafuta ugonjwa huu, wengine wao akijua wazi wako na ugonjwa huu wa virusi.

Alipoonekana kuwa ana virusi, aliingia kwa facebook yake na kuandika hivi:
 Nimepatikana niko na virusi vya UKIMWI tarehe 21 Septemba na napenda sana! Nataka kugawa ugonjwa huu kwa mfuasi yeyote, CD4 ni 971, VL ni 100,000 ni nzuri na hatari.

CD4 inaashiria wingi wa chembechembe za damu nyeupe ilhali VL inaashia kiwango cha virusi mwilini ambavyo kimsingi 100,000 ni kiwango kilichopita mpaka.

Tangu Nick ajijue ameathirika ameshawahi kufanya ngono bila kinga na zaidi ya watu ishirini.

Wengi wanalaani matendo haya lakini kama waswahili walivyosema, huwezi kulazimisha punda kunywa maji, ni kuangalia tu.
Kutana Na Wanaume Ambao Wako Tayari Kupokea Ukimwi Kutana Na Wanaume Ambao Wako Tayari Kupokea Ukimwi Reviewed by Admin on Tuesday, October 08, 2013 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.