Kampala. Klabu moja maarufu inayosifika kwa vipaza sauti na kujaa kwa mashabiki ilijionea sarakasi baada ya mashambulizi yaliyotokea hapo. Klabu hii inajulikana kama Top Pub inapatikana katika barabara ya Williams Street katikati ya jiji la Kampala. Huvutia wengi ikiwemo makahaba na walevi ambao usiku kucha hutangamana na kujibujia vinywaji na kucheza midundo ya ngoma.
Kama kawaida mambo huwa hivyo, lakini jumipili iliyopita asubuhi mambo yalibadilika. Risasi zilifyatuliwa angani na kwa waliokuwa hapo. Kila mtu alikuwa mguu niponye na mwisho wa sarakasi hio mmoja alipoteza maisha na wengine watano wanauguza majeraha waliyopata.
Ijapokuwa chanzo chake bado hakijajulikana, walioshuhudia waliiambia Daily Monitor ya kwamba kisanga hiki kilitokea baada ya wanaume wawili walipoanza kugombana kuhusu malaya mmoja.
Mlinzi mmoja aliyekataa kutajwa jina lake akihofia usalama wake anadai kuwa mmoja wa wawili hao alitoa bunduki na kuanza kufyatua risasi bila kubagua. "Kulikuwa na kizaazaa cha watu kukimbia huku na kule kuokoa maisha yao. Nilisikia watu wakipiga mayowe wakiomba msaada." aliiambia Daily Monitor.
Jamaa aliyefanya kitendo hiki yuko mbioni hajakamatwa lakini polisi wamepata sajili ya risasi zilizotumiwa na itakuwa rahisi kwao kumtambua aliyefanya kitendo hiki.
Si jambo geni kufanyika hapo klabu cha Top Pub kwani mwaka wa 2009 jeshi mmoja wa UPDF alifyatulia na kuua watu 8 baada ya malaya mmoja kumdadisi na kumuibia simu na pesa zake. Baadaye alijipiga risasi mwenyewe.

8 Washambuliwa Kwa Risasi Kwa Ugomvi Wa Kutongoza Kibiriti Goma
Reviewed by Admin
on
Tuesday, October 08, 2013
Rating:
No comments:
Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!
Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano