Unordered List

Definition List

Nyimbo Hupunguza Maumivu Mwilini, Utafiti Wasema

Kulingana na utafiti uliofanywa nchini Uingereza, imebainika kuwa asilimia 75 ya watu hutulizwa akili wakati wanaposikiliza nyimbo.

Utafiti huo ulifanya na watu kati ya umri wa miaka 16 hadi 24. Kulingana na kundi hili, wanadai kuwa nyimbo huwafanya kupunguza maumivu mwilini, utafiti uliofanywa na Lloyds Pharmacy group.

Nyimbo ambazo ziliongoza katika kupunguza maumivu na kutuliza akili ni nyimbo aina ya 'pop' ikiongoza kupunguza maumivu kwa asilimia 21, ikifuatiwa na nyimbo za 'classic' kwa asilimia 17 halafu nyimbo za 'rock' kwa asilimia 16.

Kampuni hio katika utafiti wake iliweza kutaja nyimbo ambazo zinachangia zaidi kupunguza maumivu, nazo ni:

1. Bridge Over Troubled Water (Simon and Garfunkel)

2. Angels (Robbie Williams)

3. Albatross (Freetwood Mac)

4. Candle In The Wind (Elton John)

5. Easy (The Commedores)

Utafiti huo ulifanywa kati ya watu 1500 ambao mara nyingi hukumbwa na tabu ya uchungu na uchovu mwilini.

Utafiti huo ulifanywa baada ya watu kutaka kujua umuhimu wowote wa nyimbo kwa mwanadamu.

Kampuni hio pia ilijaribu kuambia watu kuwa wasitegemee sana kutumia dawa za hospitali kwani kuna mbinu nyingine mbadala ambazo zinaweza kusitisha maumivu ya mwili.
Nyimbo Hupunguza Maumivu Mwilini, Utafiti Wasema Nyimbo Hupunguza Maumivu Mwilini, Utafiti Wasema Reviewed by Admin on Friday, October 04, 2013 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.