Kulingana na repoti iliyotolewa na shirika la World Bank, Interpol na United States, imebainika kuwa Al Shaabab wameekeza zaidi ya sh35 bilioni za Kenya ambazo zimetokana na uharamia katika uzo la miraa nchini Kenya.
Inasemekana nchi ya Kenya ndio ngome ya uchumi wa Al Shaabab huku ikiaminika kuwa kundi hilo haramu limeekeza katika kujenga majumba nchini humo. Lakini sasa imegunduliwa kuwa Al Shaabab ndio wamiliki wakubwa katika kununua na kuuza miraa.
Inaaminika kuwa Kenya inasafirisha takriban miraa zaidi ya kilo 3000 hadi Mogadishu, Somalia mara tatu kwa siku.
Pesa zinazotokana na mauzo hayo ndizo zinazotumika kuendeleza maovu katika nchi za nje ikiwemo tukio lililofanyika Westgate nchini Kenya.
Habari nyingine ni kuwa jambo hilo la Al Shaabab kuhusika na uuzaji wa miraa ndilo lililofanya nchi za Uingereza kupiga marufuku mauzo ya miraa kwa nchi yao.
Kundi la Al Shaabab ni kundi haramu ambalo linakisiwa kutaka kuleta mfumo wa kiislamu katika nchi ya Somali. Hivi majuzi walisherehekea baada ya tukio la kivamizi katika duka la Westgate.

Kenya Ndio Mdhamini Mkuu Wa Al Shaabab Kupitia Mauzo Ya Miraa/Mirungi
Reviewed by Admin
on
Wednesday, November 06, 2013
Rating:
No comments:
Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!
Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano