Klabu ya Bongo Movie ambayo inaundwa na
baadhi ya wasanii wakubwa wa filamu nchini imepasuka katikati kisa
kikidaiwa kuwa ni lile tamko linalodaiwa kutolewa na mwenyekiti wa klabu
hiyo, Vincent Kigosi ‘Ray’ kuwa mwanachama yeyote wa kundi hilo asitie
miguu kwenye mazishi ya babake Wema Sepetu, marehemu
Balozi Isaac Sepetu.
Tukio hilo la katazo lilitokea wakati wa maombolezo ya kifo cha mzee Sepetu kilichotokea Oktoba 27, mwaka huu katika Hospitali ya TMJ kwa ugonjwa wa kisukari ambapo msiba ulikuwa nyumbani kwake, Sinza Mori jijini Dar es Salaam.
Kufuatia madai hayo, baadhi ya wasanii kutoka klabu ya Bongo movies (majina tunayo) wamekuwa wakitoa lawama zao kwa Ray huku wengine wakidai wamejitoa kwenye kundi hilo kwa sababu halina umoja na limejaa unafiki.
Maneno hayo yalianza kusambaa baada ya Wema kumaliza mazishi ya babake yake Oktoba 31, mwaka huu mjini Zanzibar.
Habari za uhakika zinasema kwamba, wasanii waliotangaza kujiengua klabuni humo wameshamuomba Ray aitishe kikao cha dharura kwa ajili ya kuzungumzia hatua yake ya kuwapiga marufuku wasanii hao kutoshiriki katika mazishi ya babake Wema Sepetu huku akijua wema wa binadamu unapatikana kwenye kushiriki mazishi ya wenzake.
“Kikubwa zaidi ni kwamba, Ray wakati akisambaza zile meseji alisahau kuwa kuna siku Wema Sepetu aliwahi kuwaalika wasanii wa kundi la Bongo Muvi nyumbani kwake Makumbusho (Dar) wakala na kunywa, mbona hawakugoma kwenda?” alihoji staa mmoja aliyepinga katazo la Ray.
Maumivu makali zaidi yaliibuka kufuatia baadhi ya wasanii waliotaka kujifanya hawajapata meseji ya Ray ambapo walisema walishindwa kushiriki msiba huo kwa sababu walikuwa ‘shooting’.
“Kuna wasanii walishindwa kuweka wazi kwamba walipokea meseji ya katazo ya Ray, walipopigiwa simu na wenzao kuulizwa kwa nini hawaonekani msibani kwa Wema walisingizia eti wako location wanarekodi!
“Kwa akili za kawaida, mwenzenu kafiwa mnaweza kushikwa na ubize wa kurekodi filamu? Hawa ni wanafiki, walisingizia vile ili ionekane wana hudhuru,” alisema staa mwingine.
Baada ya hayo yote hapo tuliamua kumfuatilia kwa karibu sana mwigizaji vicent kigosi ili yujue kama madai haya ni ya kweli aua la na haya ndo baadhi ya mambo aliyoweza kuyasema Ray.
“Kawaida yangu huwa sitetemeshwi wala kuyumbishwa na maneno yamesemwa.mengi cna juu yangu lakini Mungu wa haki ananipigania….kweli nimeamini ukubwa ni jalala na nyota yangu ni kubeba mizigo ya watu. Mtasema sana Lakini Yangu Yananinyokea..." Alimaliza Ray.

Mazishi Ya Babake Wema Sepetu, Ray Ndie Aliyewazuia Bongo Movie Kutohudhuria
Reviewed by Admin
on
Friday, November 08, 2013
Rating:
No comments:
Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!
Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano