Unordered List

Definition List

Ndoa Ya Kim Na Kanye Kubutika?!? Soma Uvumi Unaotufikia Sahizi

kim kardashian na kanye west
Kama umedhania uhusiano kati ya Kim na Kanye West unaenda vyema basi wakati huu unafaa kufikiria mengine.

Kulingana na udaku unaotufikia katika blog hii kupitia Life & Style, kuna mengine fiche ambayo hayajawekwa hadharani.

Kulingana na udaku usiojulikana chanzo chake, kuna uvumi kuwa Kim yuko mikononi mwa Kanye West na hukubaliana na kile Kanye anachotaka yeye, ikiwemo siku yao ya kufanya harusi na mengineyo.

Uvumi ni kuwa Kanye ndiye anayesema yote kuhusu kujenga kwa nyumba yao mpya, lini harusi yao itafanyika na hata vile Kim anavyovalia lazima vidhibitishwe na Kanye. Kiufupi ni kuwa Kanye amechukua mamlaka yote juu ya Kim.

Pia uvumi unasemekana kuwa Kim hakuridhika na Kanye kutaka kumuoa.

"Hakuna chochote kuhusu uchumbianaji uliotokana na Kim Kardashian." udaku huo unaendelea kusema.

Pia nduguye Kim, Khloe Kardashian amekwazwa na vile Kanye anavyo muekea masharti ndugu yake.

Katka gazeti la Life & Style, Khloe analalamika  kuwa Kanye anadhani kuwa yeye ndie kila kitu, kuwa Kim ni halali yake na atamuambia kila anachotaka yeye hata wakati wa kuchagua nguo.

Si uongo kuwa Kanye West ana misimamo mikali ikizingatiwa kuwa pia anatabia ya kutishia na kutetesha watu hswa mapaparazi.

Swali ni je, wakifanya ndoa yao leo kweli itadumu?!?
Ndoa Ya Kim Na Kanye Kubutika?!? Soma Uvumi Unaotufikia Sahizi Ndoa Ya Kim Na Kanye Kubutika?!? Soma Uvumi Unaotufikia Sahizi Reviewed by Admin on Thursday, November 07, 2013 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.