MWANAMUZIKI wa Injili kutoka Kenya, Solomon Mkubwa anatarajiwa kulipamba tamasha kubwa la Hakuna Mwanamke Mbaya litakalofanyika leo Jumapili katika Kanisa la Lutherani, Mabibo-External jijini Dar.
Akizungumza na paparazi wetu, katibu wa Chama cha Waimba Injili nchini, Stella Joel, alisema lengo la tamasha hilo ni kuzindua wimbo wake wa Hakuna Mwanamke Mbaya ambao amemshirikisha Rose Mhando na wanatarajia kuwa na waimbaji mbalimbali huku mgeni rasmi akiwa ni Mbunge wa Igunga, Dkt. Dalali Kafumu.
“Watakuwepo Solomon Mkubwa, Martha Mwaipaja, Ado Novemba, Edson Mwasabwite, Martha Mlata na wengine wengi kuanzia saa nane mchana na kuendelea,” alisema Stella.
Solomon Mkubwa, Rose Mhando Kuifunika Dar Siku Ya Leo
Reviewed by Admin
on
Sunday, November 09, 2014
Rating:
No comments:
Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!
Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano