Unordered List

Definition List

Staa Wa Bongo Movies Batuli Kuolewa Very Soon

GOOD news kwa mtoto mzuri Bongo Movies, Yobnesh Yusuf ‘Batuli’ ni kwamba anatarajia kuolewa hivi karibuni baada ya kuishi maisha ya upweke kwa muda mrefu, Risasi Jumamosi linatujuza.


Batuli ambaye ni mama wa watoto wawili, ameliambia Risasi Jumamosi kuwa kwa umri alionao, amejifunza vitu vingi katika maisha hivyo kwa kuwa ameshampata mtu sahihi kwake, ameona bora aolewe. Alisema katika safari ya maisha, vikwazo ni vingi ikiwemo masuala ya skendo za wasanii lakini ameshavuka vikwazo hivyo na hahitaji tena kuyumbishwa na mtu kwani anaingia kwenye ndoa akiwa ameshajifunza mengi. “Ndoa siyo kitu cha mchezo tena kwa sisi wasanii mambo ni mengi. Kazi yetu tunakutana katika mazingira mbalimbali hatarishi na wadau tofauti, vikwazo ni vingi na mtu akivuka salama basi ni jambo la kumshukuru Mungu,” alisema Batuli.

Paparazi aliyekuwa akimhoji alimbana zaidi Batuli ili aweze kujua hiyo ‘hivi karibuni’ kwake ina maana ya lini ambapo hakutaka kutaja tarehe ya harusi lakini akaahidi kumwanika mume wake mtarajiwa Desemba 5, mwaka huu sambamba na kutaja siku husika ya ndoa. “Wewe usijali, utakuwa wa kwanza kualikwa. Tena Desemba 5 nitakuita umuone mume wangu mtarajiwa, nitakutambulisha kwa majina na kila kitu, baada ya hapo nitakupa tarehe kamili ya ndoa yangu maana kila kitu kimeshakaa kwenye mstari, soon tu nitakuwa mke wa mtu,” alisema Batuli.

Watoto wawili ambao Batuli anao kwa sasa, alizaa na wanaume wawili tofauti ambao hapendi kuwazungumzia kwa kuwa tayari zama zao zilishapita.
Staa Wa Bongo Movies Batuli Kuolewa Very Soon Staa Wa Bongo Movies Batuli Kuolewa Very Soon Reviewed by Admin on Saturday, November 22, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.