Unordered List

Definition List

Mpenzi Wa Zamani Wa Agness Masogange Afunguka Kwa Uchungu Wa Kutemwa

MCHUMBA wa Video Queen maarufu Bongo, Agnes Gerald ‘Agness Masogange’ aitwaye Evance Kom juzikati alijikuta akivunja ukimya kwa kuweka wazi kuwa msichana huyo amemsaliti baada ya kuvunja makubaliano yao.


Akizungumza na gazeti Jumatatu hii, alisema hana tena mpango wa kuoana na Agnes kwani kitendo chake cha kuamua kuhamia Afrika Kusini kimeonyesha wazi hawawezi kuishi tena pamoja. Akisimulia, Evance alisema hapo awali walikubaliana kuwa pamoja kiasi kwamba hadi kufikia kumvalisha pete, wazazi wa pande zote mbili walikwishajua na kubariki uhusiano wao.

“Wakati anapanga mipango yake ya kuhamia Afrika Kusini, hakuwahi kuniambia hata mara moja, alikuja kuniambia eti tuhamie huko siku chache tu kabla hajaondoka, nisingeweza kuondoka na kwenda kuanza maisha mapya huko wakati hapa Bongo nina miradi yangu kibao,” alisema.

Alisema kutokana na kitendo hicho cha kuhamia huko, pia mchumba wake huyo alikuwa amejiingiza kwenye mambo yasiyofaa ambayo wazazi wake wasingeweza tena kumsapoti kama angehitaji kuendelea na nia yake ya kumuoa. “Nilimpenda sana Agnes na yeye alinipenda lakini alichokiamua ni kizuri kwake, ila kwangu ni kama amenisaliti maana kajiingiza kwenye mambo yasiyofaa hivyo kwa sasa amebaki kama rafiki yangu wa kawaida tu,” alisema.

Agnes Masogange mida hii yuko nchini Afrika Kusini Akila bata na mchumba wake msauzi.
Mpenzi Wa Zamani Wa Agness Masogange Afunguka Kwa Uchungu Wa Kutemwa Mpenzi Wa Zamani Wa Agness Masogange Afunguka Kwa Uchungu Wa Kutemwa Reviewed by Admin on Saturday, November 22, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.