Mwanajeshi aliyemuua Osama bin Laden ametambulika kwa mara ya kwanza jana. Anaitwa Rob O’Neill, 38, aliyewahi kufanya mission za kijeshi zaidi ya 400.
Baba yake, Tom O’Neill anasema: “Watu wanauliza kama tunaogopa kwamba ISIS watakuja na kututeka kwa sababu Rob anafahamika sasa. Nasema nitachora target kubwa kwenye mlango wangu wa mbele na kusema ‘njooni mtuteke’.
O’Neill mwenyewe alipongezwa na rais Barack Obama kwa kumuua bin Laden kwa risasi tatu juu ya paji lake la uso wakati wanajeshi wa Marekani waliposhambulia kambi yake huko Abbottabad, May 2, 2011. O’Neill amekubali kufanyiwa mahojiano exclusive na kituo cha Fox baadaye mwezi huu.Mission zake tatu alizozifanya zimetumika kwenye filamu za action za Hollywood.
Alikuwa mwanajeshi aliyeongoza wenzie huko kuokoa meli ya Maersk Alabama, iliyokuwa imetekwa na maharamia wa Somalia ambapo operesheni hiyo ilizaa filamu ya Captain Phillips.
Mwanajeshi Aliyemuua Osama Bin Laden Ajitokeza
Reviewed by Admin
on
Friday, November 07, 2014
Rating:
No comments:
Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!
Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano