Unordered List

Definition List

Pastor Victor Kanyari Adai Amefika Level Ya Uhuru Kenyatta Na Raila Odinga Kiumaarufu Na Kifedha.

Pastor Victor Kanyari si jina geni kwa blog hii ya bkuHABARI kwani awali nishawahi kummulika na kumuorodhesha mmoja wa mapasta matapeli aka mapasta feki wanaowanyanyasa waumini wao kweupe katika makanisa.

Pasta yuyu huyu nishawahi kummulika wakati alipokumbwa na skendo la kudai kuwa anaweza kutibu ugonjwa wa UKIMWI. Well, hivi juzi Pasta Kanyari aliweza kumulikwa na mwanahabari ambaye ni mchunguzi Mohammed Ali kwa kuonyesha uovu wake anaowafanyia waumini wake.

So baada ya kumulikwa...alipata funzo ama bado anajitia hamnazo?


Kulingana na takwimu ni kuwa pasta huyu anayefahamika kwa jina la utani 'panda mbegu ya 310' anakisiwa kupokea kitita cha Ksh 1milioni kila wiki takriban milioni 20 za kibongo kila mwezi kutokana na biashara ya kanisa lake kupitia mpesa.

Hivi majuzi alipofuatwa na watangazaji wa habari alikuwa na tabasamu bila hata kuingiwa na woga wa kuangalia kamera. Mwanzo pasta huyu mwenye utata alifunguka kwa kuonyesha gari yake aina ya Range Rover Sports, gari inayomilikiwa na matajiri wachache nchini Kenya.

Pasta huyu alifunguka kuwa anashangaa kwa nini wakenya wanampa airtime ya bure, infact amejifananisha na wakuu wa Kenya kama vile Raila Odinga na Uhuru Kenyatta.

Hivi maoni yako ni yepi kuhusiana na Kanyari?
Pastor Victor Kanyari Adai Amefika Level Ya Uhuru Kenyatta Na Raila Odinga Kiumaarufu Na Kifedha. Pastor Victor Kanyari Adai Amefika Level Ya Uhuru Kenyatta Na Raila Odinga Kiumaarufu Na Kifedha. Reviewed by BkuHabari Admin on Friday, November 07, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.