Kutoka moyoni! Wakati kukiwa na maneno mengi juu ya madai ya kuvunjika kwa ndoa yake na prizenta maarufu Bongo wa Redio E-FM, Gardner G Habash ‘Kepteini’, supastaa wa Bongo Fleva, Judith Wambura Mbibo a.k.a Jide au Jaydee amefunguka kuwa naye si mkamilifu kwani siyo Yesu wala bikira Maria.
Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, wikendi iliyopita Jide aliamua kuvunja ukimya kufuatia maswali ya mashabiki wake wengi waliotaka afunguke kinachoendelea katika maisha yake.
“Watu wanategemea niwe kama Yesu au Bikira Maria? Siwezi, mimi ni mwanadamu tu. Hakuna aliye mkamilifu. Niacheni niishi maisha yangu bila stresi. Mwingine yeyote pia aishi maisha yake. Kila mmoja anatakiwa awe huru,” aliandika Jide.
Lady Jaydee: Mimi Si Bikira Maria
Reviewed by Admin
on
Monday, November 17, 2014
Rating:
No comments:
Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!
Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano