Unordered List

Definition List

Baby Madaha Na Inspekta Wanaswa Wakifanya Yao Live

Stori: Issa Mnali

Katika hali ya kushangaza, mastaa wawili wa muziki, Baby Madaha na Haroun Kahena ‘Inspector Haroun’ wamenaswa usiku wakila bata huku wakiwa kimahaba.

Tukio hilo lilinaswa na kamera ya paparazi wetu hivi karibuni kwenye pub moja iliyopo maeneo ya Kijitonyama jijini Dar ambapo awali Inspector alionekana akiwa amemkalia Madaha huku wakipigana mabusu. Baada ya paparazi wetu kujitokeza na kuanza kuwafotoa, Inspector ambaye ni mume wa mtu alishituka na kujinasua kutoka kwenye mwili wa mwanadada huyo.

Alipoulizwa juu ya kile alichokuwa akifanya wakati ni mume wa mtu, Inspector alisema: “Kaka kwani kuna kibaya gani tulichokuwa tunafanya, tupo hapa tunapanga mambo yetu ya muziki na wala hakuna ishu zaidi. ”Kwa pamoja wawili hao wakipozi kimahaba. Baby Madaha kwa sasa haijulikani anatoka kimapenzi na nani ila Inspector Haroun ni mume wa Bahati ambaye alifunga naye ndoa mwaka 2004 na wamejaaliwa kupata watoto wawili ambao ni Nassir na Shadya.

Baby Madaha Na Inspekta Wanaswa Wakifanya Yao Live Baby Madaha Na Inspekta Wanaswa Wakifanya Yao Live Reviewed by Admin on Friday, November 21, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.