Unordered List

Definition List

Aunty Ezekiel Alia Hadharani 'Location'

Hamida Hassan na Imelda Mtema


DIVA wa Filamu za Kibongo, Aunty Ezekiel hivi karibuni alijikuta akiangua kilio alipokuwa eneo la kuigiza ‘location’ pande za Kijichi jijini Dar baada ya kusumbuliwa na jino ambapo alishindwa kuvumilia maumivu.

Akizungumza na Amani baada ya kupatiwa matibabu kwenye Hospitali ya Aviation, Aunty alisema kuwa alijikuta uvumilivu unamshinda na kuangua kilio kwani kila alipojaribu kufanya kazi alishindwa.
“Huwezi amini sikupenda hata kuongea na watu, jino naliheshimu sana kwani maumivu yake kama hayajakufika unaweza kuona mtu anajifanyisha,” alisema Aunty.

Baada ya tukio hilo, Aunty aliyekuwa amejichimbia kwenye kambi ya William Mtitu amesitisha zoezi la kupiga picha hadi hali yake itakapokuwa nzuri.
Aunty Ezekiel Alia Hadharani 'Location' Aunty Ezekiel Alia Hadharani 'Location' Reviewed by Admin on Thursday, November 20, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.