Utata umetanda miongoni mwa wananchi nchini Marekani kutaka kujua ni askari yupi hasa aliyefyatua risasi iliyomuua Osama Bin Laden, zaidi ya miaka mitatu baada ya kifo cha kiongozi huyo wa kundi la kigaidi la al-Qaeda, baada ya kuibuka madai tofauti.
Askari wa zamani wa kikosi cha Seal cha wanamaji wa Marekani, Robert O'Neill, mwenye umri wa miaka 38, ameliambia gazeti la Washington Post katika mahojiano mapya kuwa ndiye alifyatua risasi iliyomuua Osama. Maelezo hayo yanapingana na yale ya Matt Bissonnette, askari mwingine wa zamani wa kikosi cha Seal aliyeshiriki katika operesheni ya kumsaka katika maelezo yaliyotolewa katika kitabu mwaka 2012.
Bin Laden, kiongozi wa al-Qaeda aliuawa mwaka 2011 katika shambulio lililofanywa na kikosi cha Seal katika makaazi yake katika mji wa Abbottabad, nchini Pakistan.Bwana O'Neill, ambaye alistaafu jeshi mwaka 2012, alilieleza hayo jarida la Esquire bila kujitambulisha. Alipangwa kujitambulisha katika mahojiano ya televisheni baadaye mwezi huu, lakini mtandao mmoja ulichapisha mapema jina la Bwana O'Neill kinyume na uamuzi wake wa kujitokeza hadharani, linaripoti gazeti la Post.
Bwana O'Neill amesema yeye pamoja na askari mwingine ambaye hajatambulishwa hadharani walipanda hadi ghorofa ya tatu katika makaazi yake huko Abbottabad, nchini Pakistan na alimwona Bin Laden akitoa kichwa nje ya mlango katika moja ya vyumba vya nyumba hiyo. Obama na timu yake ya usalama wa taifa walifuatilia shambulio hilo la Marekani katika makaazi ya Bin Laden. Komandoo ambaye hakutajwa jina, akiwa amesema katika eneo lake katika muundo wa shambulio hilo alimfyatulia risasi lakini alimkosa, kwa mujibu wa Bwana O'Neill. Hapo hapo, Bwana O'Neill alikwenda katika chumba na kumuua kiongozi wa al-Qaeda kwa kumpiga risasi kichwani, amesema.
Hata hivyo katika kitabu No Easy Day, Bwana Bissonnette amedai alikuwa mtu wa mstari wa mbele ambaye alimuua Bin Laden. Siku ya Alhamisi, Bwana Bissonnette hakupinga moja kwa moja madai ya Bwana O'Neill, katika mahojiano na shirika la utangazaji la Marekani, NBC. "Watu wawili tofauti wakieleza habari mbili tofauti kwa sababu mbili tofauti," Bwana Bissonnette aliliambia shirikahilo la utangazaji."Chochote alichosema, amesema. Sitaki kukizungumzia."
Bwana Bissonnette amepangwa kuonekana katika kipindi cha jarida la CBS dakika 60 kabla ya kuchapishwa kitabu chake cha pili, No Hero, kuhusu huduma yake katika kikosi cha Seals.Wakati huo huo anachunguzwa kwa kufichua taarifa muhimu katika kitabu chake cha kwanza, kuhusu shambuliodhidi ya Bin Laden.Taarifa kuhusu kile kilichotokea huenda isitolewe na serikali ya Marekani kwa miaka mingi.Maafisa wa wizara ya ulinzi ya Marekani hawajakanusha wala kuunga mkono maelezo ya Bwana O'Neill, lakini wiki iliyopita, viongozi waandamizi wa operesheni maalum walituma barua kwa askari wote wa kikosi cha wanamaji cha Seals wakiwataka kuheshimu maadili ya kazi yao kwa kutotoa taarifa za operesheni za kikosi hicho, ikiwa ni pamoja na kuepuka kutafuta umaarufu wa umma"."Hatutakiwi kufungamana na ubinafsi na kupuuza maadili yetu kwa kutafuta umaarufu wa umma na kujinufaisha kifedha," waliandika katika barua hiyo.Bin Laden alithibitika kuuawa katika shambulio hilo na mwili wake ulizikwa baharini.Giza na msongamano wa nyumba katika makazi hayo kumefanya baadhi ya askari wa kikosi cha Seals kuhoji kama inawezekana kubaini ni risasi za nani
Jina La Aliyemuua Osama Bin Laden Sasa Lazua Utata
Reviewed by Admin
on
Saturday, November 08, 2014
Rating:
No comments:
Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!
Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano