Unordered List

Definition List

Penzi La Ray Lawafanya Johari Na Chuchu Hans Kuwa Pamba Na Moto

Stori: Mayasa Mariwata

STAA wa filamu Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’ amesema kwa sasa hataki kabisa kusikia habari za mwigizaji, Chuchu Hans ambaye wamekuwa wakitifuana mara kwa mara wakidaiwa kugombea penzi la Vincent Kigosi ‘Ray’.

Akikitemea cheche kinasa sauti cha paparazi wetu baada ya kuulizwa kuhusiana na hatma ya malumbano yao ya mara kwa mara na Chuchu, Johari alisema hataki kumzungumzia mwanadada huyo kwani anampaisha bure.

“Nimeamua nikae kimya kabisa wala sitaki kuzozana na mtu nitajishushia hadhi kwa mashabiki wangu bure, siwezi kuwa namnufaisha mtu kwa kumpandisha daraja kupitia mgongo wangu kutokana na malumbano,” alisema Johari.
Penzi La Ray Lawafanya Johari Na Chuchu Hans Kuwa Pamba Na Moto Penzi La Ray Lawafanya Johari Na Chuchu Hans Kuwa Pamba Na Moto Reviewed by Admin on Monday, November 10, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.