Unordered List

Definition List

Msanii Wa Bongo Movie Anaswa Makaburini Akifanya Matambiko Ya Kichawi

Stori na picha: Global Publishers


Ulozi! Chipukizi sinema za Kibongo, Fatuma Ayubu ‘Fetty’ amenaswa makaburini akiwanga katika kile kinachodaiwa kuwa ni kutekeleza masharti ya ‘sangoma’ ili ajipatie umaarufu na kuwafikia mastaa kama Wema Isaac Sepetu, Jacqueline Wolper Massawe na Elizabeth Michael ‘Lulu’.

Kwa mujibu wa shuhuda wetu, tukio hilo lilijiri wikiendi iliyopita kwenye Makaburi ya Ufi yaliyopo maeneo ya Ubungo-Kisiwani jijini Dar, mishale ya saa nne usiku.

Habari zilidai kwamba msanii huyo alifumwa akivunja nazi na kuzungumza maneno yasiyoeleweka. Awali, ilidaiwa kwamba, Fetty ambaye anaonekana kwenye Filamu ya House of Death akiwa na mwigizaji Kulwa Kikumba ’Dude’ alitinga kwenye makaburi hayo akiwa ameshika kimfuko huku akiangaza huku na huku kisha akatoa nazi na kuivunja huku akinuiza maneno bila kujua kuna mtu alikuwa akimpiga picha....

Ijumaa Wikienda lilipomtafuta Fetty na kumuuliza juu ya madai hayo, alianza kujikanyaga kabla ya kufunguka kuwa hapendi mambo ya kishirikina ila alilazimika kufanya hivyo kutokana na masharti aliyopewa na mganga wake kutokana na matatizo yake ya kimaisha yanayomsumbua pamoja na ndoto yake ya kuwa msanii mkubwa.

Picha alizonaswa na paparazi katika tukio zima:





Msanii Wa Bongo Movie Anaswa Makaburini Akifanya Matambiko Ya Kichawi Msanii Wa Bongo Movie Anaswa Makaburini Akifanya Matambiko Ya Kichawi Reviewed by Admin on Monday, November 24, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.