Ukiskia mtu analalamika kuhusu ndege yenye tashwishi, fikiria ndege ya US Airways ambayo ililazimika kutua kwa dharura baada <more!> ya mbwa kumwaga kinyesi kwa ndege mara mbili wiki iliyopita.
Cheki video ya mahojiano:
Ndege hio ilikuwa shwari kabla abiria kuanza kunusa harufu chafu ambayo ilinuka kama kinyesi cha mbwa.
"Baada ya kusafiri kwa saa moja hivi, nilianza kunusa harufu nzito chafu" Steve McCall alikuwa akihojiwa.
"Niliangalia mbele nikamwona mbwa mkubwa futi 3, 4 hivi urefu akimwaga kinyesi bila wasiwasi"
"Abiria wengine walianza kurusha tweets kwa mtandao kuashiria tukio hilo huku wahudumu ndani ya ndege hio wakifanya usafi...harufu hio ilitapakaa ndege nzima" Steve aliongezea.
Baada ya saa moja nyingine bado harufu ilikuwa mbichi. Kutia kidonda msumari wa moto, mbwa huyo akaanza kumwaga kinyesi kwa mara nyingine.
Hii ililazimisha rubani kufanya emergency landing sababu wahudumu wa ndege hio waliishiwa na vifaa vya kusafisha uchafu huo.
Mmiliki wa mbwa huyo hakuwasaza abiria kwani aliomba msamaha na kuwataka kila mmoja atoe anwani yake ili ampe starbucks gift cards kama njia ya kutoa pole kwa wote waliochefuka.

Kinyesi Cha Mbwa Chamfanya Rubani Wa Ndege Kulazimisha Ndege Kutua Kwa Dharura
Reviewed by Admin
on
Saturday, June 07, 2014
Rating:
No comments:
Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!
Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano