Unordered List

Definition List

Watanzania Wazivuruga Akaunti Za BET



Hii sasa ni shida!!! Huenda wafanyakazi wa kituo cha BET, kama hawatakuwa wanajichekea tu kwa jinsi wabongo walivyo na fujo kwenye ukurasa wao wa Facebook na Instagram, basi watakuwa wanajuta kumtaja kwenye tuzo hizo.Katika utaratibu wake wa kuweka picha za nominees mbalimbali wa tuzo hizo kupitia mitandao ya Instagram na Facebook, BET wamejikuta wakishangaa na namna ambavyo jina la Diamond limekuwa likitajwa katika asilimia kubwa ya comments hata kwenye picha zisizomhusu staa huyo wa Tanzania.

Hiyo ni kutokana na kampeni iliyoanzishwa na mashabiki wa muimbaji huyo wanaoitaka BET ifahamu nguvu yake. Kwa wengine comments hizo zimeanza kuwa kero kwenye ukurasa huo japo BET wanaweza kufurahia jambo moja kubwa – wamepata followers wengi kutoka Tanzania.

Pamoja na kwamba comments hizo zinaweza zisiwe na mchango wowote wa kumfanya ashinde, kituo hicho cha BET kinapata ujumbe muhimu kuhusiana na kukubalika kwake Afrika Mashariki.

Ujumbe huo unaweza kuwa mwanzo mwingine wa Diamond kupata airtime kwenye kituo hicho kwa video zake zinazokuja hasa ya wimbo aliomshirikisha Iyanya ambayo video yake ilifanyika nchini Uingereza mwezi uliopita.

Ujumbe mwingine jumuiya ya muziki wa kimataifa inaoupata kupitia mashambulizi hayo ya mashabiki wa Diamond, ni ukubwa na ushawishi alionao hitmaker huyo wa My Number 1.

Haya ni baadhi ya maoni ya wabongo kwenye picha za Instagram za mastaa wengine yanayomhusu Diamond.

jandareal Yupo kwenye best actor pia? Bet watakuwa wanajichekea

tutwissyben Wabongo nomaaa kila sehemu ni sisi,,,wataisoma D’s tym iwe movie, music ni #diamondplatnumz

nico_agust@twissyben shida tupu!! hapa lazma watuone kuwa tuna uelewa mdogo wa mambo haya!!

jusseee Hahhah siwanesema akuna kura bat mtu akiongelewa Sana ila sisi noma ata kwa washereheshaji atujali no daimondplatnomz tu ata kwenye movie ivyo ivyo kweli watatupa tu tuzo na kutujua atujielewi. Unazani uwongo kweli wataangalia kahistoria ketu watatupa tu tuzo ole wao wachakachue tunamtuma kikwete nikuandamana mwanza mwisho kwa hali hii kila kit BMT ni diamond tu watunyime tuzo sasa waone

salmaasaidyHahahahahahaha nyamani mi nacheka sana kila post @diamondplatnumz .nimecheka kweli @jusseee

janeelingerie Hahahaaaaaa uuuuwiii nacheka balaa daaahh kweli watu hawaelewi daaahh ila @diamondplatnumz uko juu hata hawa jamaa wataashangaa @wemasepetu

berthamagodi Kashapata umaarufu jamaa mana kila mtu atataka amjue mana kachafua mbaya wabongo tumetisha aiseee

jandareal Dah lkn licha ya kupata umaarufu pia itaonyesha ni kiasi gan wabongo tunaakili nzito. Aliyetoa instruction kufanya haya alikosea sana, sema bado tunahitaji elimu juu ya hili,jishtukien had movie mnacoment diamondplatnumz @diamondplatnumz tolea ufafanuzi wa hili

berthamagodi Shida tunakurupuka hao wahusika walito bio tuingie kupiga kura kumbe kituo cha redio pia kule diom kashine mbaya sasa uku ndo kafunga kaz marekan nzima watakua wanashangaaa. Bongo noma sana

rehemaessy Wapenzi wa dai kuweni waelewa jazeni ktk picha ya dai sio kila picha mnatuzalilisha wabongo inaonekana hatujui kusoma @desmondmshana @thatgud_girl_g @mnayanda waelewesheni na wenzenu

telhom Guys nendeni kwa picha ya Diamond ndo mukaandike jina lake la hasha mkiandika hapa nikujisumbua hii si picha yake so hawatoihesabu please go back to @betawards then chagua jina la @diamondplatnumz ndo uandike jina lake mbona mko wagumu kuelewa jamani

nakupendapia Tanzanians I love the way you g got @diamondplatnumz back. But na hope mnavote kwenye bet website coz the kelelehere doesn’t really count.

magazinequeendrika Y’all. There is nothing you can say to convince BET to get this man to perform. They made this decision months ago, so stop trying!!!!!

Katika hatua nyingine, kituo cha redio cha Kenya cha Home Boyz Radio jana kilitaka kujua muziki wa nani kati ya Diamond na Davido unaopendwa zaidi na Wakenya. Tweets hizi zinaongea zenyewe.

Bongo5
Watanzania Wazivuruga Akaunti Za BET Watanzania Wazivuruga Akaunti Za BET Reviewed by Admin on Thursday, June 05, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.