Unordered List

Definition List

Nyimbo Mpya Za Ali Kiba Zachoma Server Za Mkito.com, Mtandao Wazimika Kwa Muda


Siku ya jana 25/7 ilikuwa buzy sana kwa Ali Kiba na pia kwa mtandao wa mkito.com ambao unajulikana kuuza nyimbo za wasanii nchini Bongo baada ya staa huyu wa Dushelele kuachilia vibao viwili wakati mmoja.

Kwa sapraiz ambayo haikutarajiwa kamwe, mtandao huo uliweza kupata watembeleaji wengi aka traffic kiasi cha kuufanya kuzimika na kuingia offline.

Baada ya Alikiba kuweka wazi kuwa ameweka vibao vyake viwili kwa huo mtandao, wengi walikimbilia kupata kuwa wa kwanza kudownload na kusikiliza ngoma zenyewe za 'mwana' na 'kimasomaso'.

Siku ya jana nyakati za asubuhi ilikuwa hauwezi kabisa kuuingia mtandao huo.

Inaonekana Alikiba alitumia promo kali kuuza ujio wake upya kwa kufufua bifu lake na Diamond Platnumz.

Kama bado hujaskiliza ngoma zenyewe ingia udownload hapa
Nyimbo Mpya Za Ali Kiba Zachoma Server Za Mkito.com, Mtandao Wazimika Kwa Muda Nyimbo Mpya Za Ali Kiba Zachoma Server Za Mkito.com, Mtandao Wazimika Kwa Muda Reviewed by Admin on Saturday, July 26, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.