Mji wa Wenzhou uliamka leo asubuhi kupata mto ambao wamekues wakiutumia kila siku umebadilika rangi ya damu. Kulingana na wakaazi wa sehemu hio wamedai kuwa mto huo saa kumi za usiku ulikuwa uko sawa lakini kufikia saa 12 asubuhi mto huo ulibadilika rangi yake kuwa damu.
Mkaazi mzee aliyeishi mji huo maisha yake yote amefunguka kuwa tukio hilo halijawahi kutokea kamwe sehemu hio.
Kulingana na wanasayansi wamedai kuwa tukio hilo limechangiwa na uchafuzi wa mazingira na imewabidi kuchukua sampuli ili kufanya uchunguzi zaidi.
Mji wa Wenzhou unafahamika sana na unapatikana East China katika mkoa wa Zhejiang Province.
Watafiti washabaini kuwa tukio hili linaletwa na mmomonyoko wa udongo.
Lakini kwa mtandao watu wana maoni tofauti haswa wengine kudai kuwa hio ni dalili ya mwisho wa dunia.
Tisha: Mto Wajeuka Rangi Ya Damu, Watu Waingiwa Na Woga Kuwa Ni Mwisho Wa Dunia
Reviewed by Admin
on
Sunday, July 27, 2014
Rating:
No comments:
Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!
Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano