Unordered List

Definition List

Mdada Atumia Zaidi Ya $31,000 Ili Kufanana Na Kim Kardashian

Najua ulipata kuisoma stori ya Toby Sheldon ambaye alitumia zaidi ya dola 100,000 kufanana na Justin Bieber lakini aliishia kuwa kama shetani, well roundi hii utaipenda ya huyu mdada anayejitengeneza kufanana kama Kim Kardashian.

Claire Leeson mwenye umri wa miaka 25 kutoka Great Britain anatamani kufanana kama mpenzi wa zamani wa Ray J aliyetoa naye video ya ngono, Kim Kardashian.

Hadi wa sasa ashatumia zaidi ya $31,000 ili kuipata shepu ya Kim.

Jambo la kwanza Leeson alilolifanya nikuhakikisha amefanya meno yake kuwa meupe kama ya Kim na sasa anajitayarisha kuitengeneza sekta muhimu ya 'Kim Kardashian'

"Sasa nataka matiti yangu yaekwe level moja na ya Kim Kardashian." Leeson aliliambia gazeti la The Daily Mirror.

Leeson pia amekuwa akijitwika na kununua make up, nywele na vipodozi vinavyohusiana na nywele ambazo Kim Kardashian hutumia.

Leeson aliongezea kuwa yeye huvalia makalio ya mchina (silicon implants) lakini sahizi anafanya utafiti wa kutengeneza makalio originally.

Jambo lilimfanya kuchukua mwondoko huu ni kuwa Leeson amedai kuwa alipokuwa shuleni alikuwa akipewa kila aina ya majina na kuitwa kuwa yeye ni ugly.

Hivi kweli ana sura mbaya ama ni yeye mwenyewe hajiamini
Mdada Atumia Zaidi Ya $31,000 Ili Kufanana Na Kim Kardashian Mdada Atumia Zaidi Ya $31,000 Ili Kufanana Na Kim Kardashian Reviewed by Admin on Tuesday, July 15, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.