Unordered List

Definition List

Aunt Ezekiel Adai Kuwa Hana Nyota Mbaya Na Wanaume Kama Inavyodaiwa


Baada ya kudaiwa kuwa na gundu kufuatia kila mwanaume anayeishi naye kuandamwa na majanga, staa wa Bongo Movies, Aunt Ezekiel Grayson ameibuka na kukanusha madai hayo akisemahayana ukweli.

Baada ya maneno hayo kutua katika dawati la Ijumaa Wikienda, wanahabari walimsaka Aunt ili kumsikia anazungumziaje taarifa hizo ambapo alitiririka: “Sina gundu na wanaume jamani, uzuri ni kwamba kila niliyeishi naye kulikuwa na sababu za msingi za kuachana. Siyo Jack Pemba wala Hartmann(Mbilinyi).

“Watu wanazungumza tu bila kujua ukweli, hata kwa Sunday Demonte (mumewe wa sasa), yupo vizuri na hajafungwa kama wanavyosema,” alisema Aunt.

Miongoni mwa wanaume walioogelea katika penzi la Auntkisha kumwagana kwa sababu tofuati ni pamoja na Mwilu Mwilola ‘Silvanus’, Hartman na Jack Pemba.
Aunt Ezekiel Adai Kuwa Hana Nyota Mbaya Na Wanaume Kama Inavyodaiwa Aunt Ezekiel Adai Kuwa Hana Nyota Mbaya Na Wanaume Kama Inavyodaiwa Reviewed by Unknown on Monday, July 14, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.