Unordered List

Definition List

Wema Sepetu Afunguka Kwa Risasi Kuwa Amemsamehe VJ Penny

STAA wa sinema za Kibongo, Wema Sepetu amesema baada ya kutokuwa na maelewano kwa muda mrefu na mtangazaji maarufu Bongo, Peniel Mungilwa ‘Penny’, sasa ameamua kumsamehe rasmi kwa heshima ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, Wema alisema: “Kwa moyo mweupe, nasema nimemsamehe Penny, hata nikikutana naye popote nitasalimiana naye kama kawaida.


Nimeamua kuachana na yote, mimi ni binti wa Kiislam na nahitaji sana swaumu yangu ipokelewe vyema kwa Mungu.

Kwa upande wa Penny alifunguka: “Siwezi kusema nitamchukia Wema ila nimekubali matokeo, sina tatizo naye tena ingawa najua hatuwezi kuwa marafiki tena kama zamani, lakini yaliyopita yameshapita.”Wema na Penny walikuwa na bifu kwa muda mrefu, chanzo kikiwa Penny kuingilia uhusiano wa Wema kwa Mwanabongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Wema Sepetu Afunguka Kwa Risasi Kuwa Amemsamehe VJ Penny Wema Sepetu Afunguka Kwa Risasi Kuwa Amemsamehe VJ Penny Reviewed by Unknown on Wednesday, July 16, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.