Unordered List

Definition List

Ray C Atafuta Mbinu Ya Kumnasua Diamond Platinumz Kutoka Kwa Wema Sepetu

Msanii "kiuno bila mfupa" Rehema Chalamila. 'Ray C' anadaiwa kuwa bize na harakati za kumnasa sukari ya warembo Diamond Platinumz katika anga za maoenzi huku duru za habari zikidai kuwa muda si mrefu kuanzia saaa yataandikwa mengi juu ya wawili hao

Mwandishi wetu alizungumza na rafiki wa karibu na Ray C hivi karibuni na kuambiwa kuwa muda mwingi jina la Diamond halikatiki mdomoni mwa mrembo huyo

Chanzo chetu cha habari kilizidi kudai kuwa kwa sasa Ray C hana furaha hadi atakapotimiza nia na lengo la kumnasa Diamond hapo ndipo furaha yake itakapotimu


Aidha habari zinazidi kudai kuwa mara kadhaa Ray C amekuwa akipanga Miadi ya kukutana na Diamond licha yakushindikana kwa apointiment hizo kila mara "kwasasa Ray C haambiwi kitu kwa Diamond, ana haha kila wakati kumweka mikononi mwake, hana furaha kabisa hadi lengo lake litakapotimia, na muda si mrefu mtaandika juu ya hao" alisema rafiki ea Karibu na Ray C

Mwandishi wetu aliwatafuta wawili hao kwa njia ya simu ambapo simu ya Ray C ilionekana kuwa bize muda mwingi huku Diamond akidai kutokuwa na taarifa juu ya madai hao "kaka mimi sina taarifa kabisa na habari hizo, kwangu Ray C namchukulia kama dada yangu" alisema Diamond.
Mwandishi wetu alipomtaka Diamond kufafanua hatua atakayochukua endapo mrembo huyo ataamua kumwambia anamtaka ambapo kwa haraka Diamond alisema "NO COMNENT (sina cha kujibu)"  na kukata simu.

Credit: Swahilitz
Ray C Atafuta Mbinu Ya Kumnasua Diamond Platinumz Kutoka Kwa Wema Sepetu Ray C Atafuta Mbinu Ya Kumnasua Diamond Platinumz Kutoka Kwa Wema Sepetu Reviewed by Admin on Sunday, March 23, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.