Unordered List

Definition List

Bifu La Irene Uwoya Na Jackline Wolper Latatuliwa

Ule ugomvi  uliokuwepo kwa takribani miaka miwili  kati ya mastaa wakubwa na warembo Jackline Wolper na Irene Uwoya hatimaye umefikia tamati baada ya kupatanishwa juzi. 

Wawili hao walidaiwa kuingia katika beef zito baada ya Uwoya kumsema Wolper vibaya kwenye media ambapo pia aliwahi kukaririwa na gazeti moja akiwa jijini Arusha akisema kuwa Wolper amemroga ili amshushe kwenye sanaa na yeye(Wolper) kuwa juu kisanaa kitu ambacho kilidaiwa kumuudhi sana Wolper.

Chanzo kimoja kilicho karibu na mastaa hao kikizungumza na Swahiliworldplanet  kilisema kuwa aliyewapatanisha ni Steve Nyerere na wote wawili wakakubali kuondoa tofauti zao.

"Wolper na Irene Uwoya wameitwa na kupatanishwa na Steve Nyerere sasa wako poa, unajua Wolper alikasirishwa na kitendo cha Uwoya kwenda kwenye media na kumchafua kwa mambo ambayo hakufanya kipindi cha nyuma" kilisema chanzo hicho huku kikikataa kuwekwa jina lake kweupe.
Bifu La Irene Uwoya Na Jackline Wolper Latatuliwa Bifu La Irene Uwoya Na Jackline Wolper Latatuliwa Reviewed by Admin on Friday, March 28, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.