Unordered List

Definition List

Picha: Shilole Na Serengeti Boy Katika Mahaba Mazito

KWA mara nyingine, staa anayekimbiza kwenye filamu na muziki wa mduara, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ au ‘Shishi’ ameibuka katika penzi jipya na bwana mdogo anayechipukia katika muziki wa Bongo Fleva, Nouh Mziwanda, Risasi Mchanganyiko limeinasa.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, Shilole kwa sasa hasikii wala haoni kwa Nouh pamoja na kwamba wawili hao wanaonekana kuwa na tofauti kubwa ya kiumri , Shilole akionekana kuwa mkubwa zaidi ya Nouh.

“Shilole ni kama anambemenda  Nouh lakini ndiyo hivyo, haoni wala hasikii, kila siku wako pamoja kama kumbikumbi,” kilisema chanzo chetu.

Waandishi wetu waliwafuatilia wawili hao kwa nyakati tofauti na kufanikiwa kuzinasa picha zao walizozipiga katika mikao ya kimahaba.

Baada ya kuzinasa picha hizo, waandishi  wetu walimtafuta  Nouh na kumweka mtu kati kuhusu uhusiano wake na Shilole.

“Ni kweli ninatoka na Shilole ni mpenzi wangu na sidhani kama nitakuja kuachana naye maana tunapendana sana na nimevutiwa na mavituz yake,” alisema Nouh.

Kuhusu tofauti ya umri wake na ule wa Shilole, Nouh alisema umri huwa haumati katika mapenzi.

“Mapenzi ni mapenzi na umri utabaki kuwa namba tu, ni vyema  mtu ukaongozwa na hisia zako kuliko kuhofia umri wa mtu ndiyo maana miye ninakula vinono,” alisisitiza.

Pia, Nouh alisema hakutarajia kukubaliwa na  Shilole baada ya kumtokea walipokutana  katika  studio moja jijni Dar na sasa wamekolea kwenye penzi motomoto.



“Nampenda Shishi, nafanya kila njia nimshawishi awe mke wangu wa ndoa,” aliongeza.
Hata hivyo, Shilole alipozungumza na waandishi wetu alipatwa na  kigugumizi kukubali uhusiano wake wa kimapenzi na kinda huyo wa Bongo Fleva.

Shilole alisema Nouh ni rafiki yake kama walivyo marafiki zake wengine.

Waandishi wetu walipomuonesha picha zao walizokuwa wamekaa katika mikao ya  kihasarahasara, Shilole aliangua kicheko na kisha akasema:

“Mh! Sina la kuwajibu kama picha zinasema mimi na Nouh ni wapenzi haya.” 

Hii siyo mara ya kwanza kwa Shilole kuripotiwa kutoka na Serengeti Boy,
Picha: Shilole Na Serengeti Boy Katika Mahaba Mazito Picha: Shilole Na Serengeti Boy Katika Mahaba Mazito Reviewed by Admin on Thursday, March 27, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.